Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali yasioambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kituo Cha Afrika cha Usimamizi wa Udhibiti na Uzuizi wa Magonjwa (CDC)Dkt,Ahmed Ubwe akitoa hotuba katika Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali yasio ambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali yasio ambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali yasio ambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
*********************
NA SABIHA KHAMIS MAELEZO ZANZIBAR 15.08.2022
Waziri wa Afya Mh. Nassor Ahmed Mazrui amesema Shirika la Udhibiti na Usimamizi wa Magonjwa ya Mripuko CDC wameihakikisha Sekta ya Afya kuwa wataendeleza ushirikiano na nchi za Afrika Mashariki ili kuweza kujikinga na maradhi ya mripuko ikiwemo Kipindupindu ,Uviko- 19 na Ebola.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano uliowashirikisha Mawaziri wa wizara ya Afya kutoka nchi mbali mbali za Afrika Mashariki, huko ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni Zanzibar, Waziri Mazrui amesema mashirikiano yaliopo kati yao na shirika hilo yatasaidia kuyapatia ufumbuzi maradhi hayo.
Aidha amesema kupitia mkutano huo utasaidia kujenga mfumo mpya wa kuimarisha mashirikiano kati yao na umoja wa nchi za Afrika Mashariki katika sekta ya Afya .
Alifafanua kuwa Mkutano huo utawanufaisha na kuwapatia maudhui mazuri watendaji wa Sekta ya Afya ili kuweza kukabiliana na maradhi hayo pindi yanapotokezea katika nchi zao.
“azma ya mkutano huu ni kuziwezesha Nchi za Afrika Mashariki kuweza kujikinga na maradhi ya mripuko kutoka nchi moja kwenda nyengine” alisema Waziri Mazurui
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Udhibiti na Usimamizi wa Magonjwa ya Mripuko (CDC) Dk. Ahmed Ubwe amesema wapo tayari kufanya kazi kwa mashirikiano kati yao na Nchi Jirani za Afrika Mashariki ili kuwasaidia kujikwamua katika maradhi hayo.
Mkutano huo ni wa siku mbili ukiwashirikisha wadau wa Afya kutoka Nchi Mbalimbali za Afika Mashariki ikiwemo Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia na nchi nyengine jirani.