Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akihutubia katika ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa Sabato Magomeni iliyofanyika Kwembe Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiteta jambo na Mchungaji Fidelis Mngwabi (katikati) kabla ya ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa Sabato Magomeni iliyofanyika Kwembe Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akipokea vitabu kutoka kwa Mchungaji Marko Barnabas, (kushoto) baada ya ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa Sabato Magomeni iliyofanyika Kwembe Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akipanda mti baada ya ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa Sabato Magomeni iliyofanyika Kwembe Jijini Dar es Salaam.
……………………………….
Waumini waombwa kuiombea nchi dhidi ya majanga mbalimbali likiwemo janga la njaa, changamoto za kiuchumi zinazo sababishwa ama na sisi wenyewe au mataifa mengine, magonjwa, dhiki na mmomonyoko wa maadili.
“Uwekezaji katika familia imara ni jambo la msingi, bila kwekeza katika familia hakuna nchi hakuna mataifa hakuna dunia.Msukumo wa watu wanaosimamia dhambi kutumia rasilimali fedha kwenye mambo maovu ni mkubwa kuliko msukumo wa kutetea mambo mema.”
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa sabato Magomeni Mwaka 2022, Kwembe Jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na Kauli mbiu “NITAKWENDA KWA NGUVU ZA MUNGU.”
Amefafanua kwamba pamoja na kumtegemea Mungu, bado maandiko matakatifu yanatuhimiza kufanya kazi kwa bidii. Katika hili niendelee kuwasihi ndugu Waumini kufanya kazi kwa bidiii huku tukimtumainia Mungu na kuomba baraka zake katika kila kitu. Licha ya kwamba nchi yetu haiegemei upande wowote katika masuala ya dini (Secular State) lakini sehemu kubwa ya watu wake wanaamini katika Mungu kupitia dini na madhehebu mbalimbali.
“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Sekta ya elimu kupitia taasisi zake za elimu; Sekta ya afya kupitia hospitali na vituo vya afya; pamoja na Sekta ya habari kupitia vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa. Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ustawi wa taasisi hizo ili ziendelee kuwa sehemu ya kuliletea maendeleo Taifa letu.”
Naye Mchungaji Fidelis Mngwabi, Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati mwa Tanzania (ECT), katika neno lake la shukrani ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wa kanisa la waadventista wa Sabato katika kulinda umoja amani na Upendo.
“kanisa litaendelea kuwa na msimamo wa Mungu katika kusaidia waumini kwenda katika njia iliyo sahihi.”