
Vijana wa UVCCM kata ya Buswelu wakiwa katika matembezi ya kuhamasisha zoezi la Sensa ya watu na makazi


Vijana wa UVCCM kata ya Buswelu waliojitokeza kushiriki matembezi kwaajili ya kuhamasisha zoezi la ushiriki wa Sensa ya watu na makazi Kwa makundi maalum
*************************
Makundi maalum ikiwemo watu wenye ulemavu wametakiwa kuhakikisha wanashiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajia kufanyika mwezi Agosti 23 mwaka huu Ili kuisaidia Serikali kupata takwimu sahihi zitakazosaidia kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama Cha mapinduzi kata ya Buswelu Ndugu Josephat Mazuri wakati wa matembezi maalum yenye lengo la kuhamasisha jamii kushiriki zoezi hilo huku akiiasa kuhakikisha watu wenye ulemavu, watoto, wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuhesabiwa
‘ .. Watu wenye ulemavu wasifichwe, Wanawake wawe mstari wa mbele katika hili, jambo lolote likisimamiwa vizuri lazima lifanikiwe ..’ Alisema
Aidha Mwenyekiti Mazuri akafafanua kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kuendesha zoezi hilo hivyo amewaomba wananchi kuhakikisha wanamuunga mkono Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Kwa kuhakikisha wanahesabiwa ifikapo siku hiyo
Nae Katibu wa jumuiya ya vijana ya chama hicho Ndugu Manyanya Sayigilya akasema kuwa vijana wa kata ya Buswelu wataendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo huku akiwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe Hassan Elias Masalla Kwa jitihada zao katika kuwatumikia wananchi wanaowaongoza na kuwaletea maendeleo
Wakumele Kafugugu ni miongoni mwa vijana walioshiriki matembezi hayo ambapo amewapongeza viongozi wa jumuiya ya vijana wa chama Cha mapinduzi kata ya Buswelu Kwa kuamua kuja na mbinu mbadala katika kuhamasisha jamii kushiriki Sensa lakini pia kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo zinazofanywa na Serikali ya chama Cha mapinduzi