Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizindua mitambo ya kisasa ya uchorongaji na uchimbaji madini ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 wakati wa hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse juu ya mitambo ya kisasa ya uchorongaji na uchimbaji madini ya Shirika hilo mara baada ya kuizindua wakati wa hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika leo Agosti 12,202 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akizungumza na viongozi, wadau wa sekta ya madini, watumishi pamoja na wananchi mbalimbali waliohudhuria hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse,akitoa taarifa ya shirika hilo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Seif Gulamali,akitoa pongezi kwa STAMICO wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua mkaa mbadala (Rafiki Briquettes) ulioanzishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uwekezaji katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightness Mauki akipokea mfano wa hundi ya Sh bilioni 2.2 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo ikiwa ni gawio kwa Serikali iliyokabidhiwa jana jijini Dodoma wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya STAMICO. Anayeshuhudia katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk Venance Mwasse.
…………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Mpango,ameitaka Wizara ya Madini, STAMICO na NEMC kuongeza kasi ya ukaguzi wa migodi na midogo ili kubaini na kudhibiti uharibifu wa mazingira.
Makamu wa Rais amesema hayo leo Agosti 12, 2022 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)
Amasema elimu ya kutosha inapaswa kutolewa juu ya madhara makubwa ya uchafuzi wa mazingira kwa maisha ya binadamu na viumbe vingine hai na uendelevu wa ikolojia.
Kwa upande wake Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema shirika la madini la taifa STAMICO linapaswa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza ushindani duniani na sio Tanzania pekee.
Aidha Waziri Biteko ameipongeza STAMICO kwa ubunifu wakati wa kukabiliana na changamoto za taratibu za manunuzi zilizokuwa zinajitokeza.
” Mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya shirika hilo ndio yameleta mafanikiao ambapo zaidi ya ajira 700 zimezalishwa ndani ya mgodi wa Kiwira.”amesema Dk.Biteko
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,ameitaka STAMICO kuongeza uzalishaji wa Mkaa mbadala na kusambaza kwa wananchi ili kutunza mazingira huku akizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa STAMICO katika utunzaji wa mazingira.
”Nawaasa kuhakikisha uzalishaji wa mkaa huo unaongezeka ili watanzania waweze kutumia na kusaidia katika utunzaji mazingira.”amesema Dkt.Jafo
Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya STAMICO Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Venance Mwasse,amesema shirika limefanikiwa kufufua mgodi wa Kiwira ambao ulikufa toka mwaka 2012 ambapo kwa sasa unaendelea nashughuli zake kama kawaida pamoja na kusaini mkataba wa kuuza makaa ya mawe elfu sitini yenye thamani ya shilingi bilioni nne.
”STAMICO inatarajia kununua mitambo kumi kwa ajili ya wachimbaji wadogo pamoja kuendelea kuwasaidia wachimbaji wenye mahitaji maalumu.”amesema Dkt.Mwasse