Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Doto Biteko,wakiongoza matembezi kutoka eneo la Hoteli ya Royal Village kuelekea Ipagala ambako kulifanyika zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati) akishiriki mazoezi ya viungo na viongozi wengine kulia Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Doto Biteko na Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyamule wakati wa uzinduzi wa ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma leo Agosti 11,2022 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akzungumza wakati wa wakati wa uzinduzi wa ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse akitoa neno la utangulizi wakati wa wakati wa uzinduzi wa ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma leo Agosti 11,2022 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizindua Kampeni ya ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyoambatana na tukio la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
…………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhusisha masharti ya upandaji miti kwa vibali vya ujenzi.
Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 11, 2022 wakati akishiriki uzinduzi wa kampeni ya ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyokwenda sambamba na zoezi la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ambapo imepandwa miti 540 katika eneo hilo kati ya 2,000 itakayopandwa Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)
Dk.Jafo amesema kuwa ili kuwa na dhamira ya dhati katika utunzaji wa mazingira na kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika zinazoyakabili maeneo mbalimbali nchini wakurugenzi wanapogawa viwanja wahakikishe vinakuwa na eneo la kupanda miti.
“Natoa maelekezo kwa wakurugenzi wote ndani ya Tanzania kuwa mnapogawa viwanja vya watu kwenda kujenga nyumba, vibali vya ujenzi lazima alete ramani ya jengo inayoonyesha miti mingapi itapandwa”amesema Waziri Jafo
Dkt. Jafo ameipongeza Wizara ya Madini na shirika hilo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira.
“Niwapongeze STAMICO kwa kuja na kampeni hii ambayo itatusaidia katika kuifanya Dodoma na mikoa mingine kuwa ya kijani na mnaonesha kuunga mkono juhudi za viongozi wetu wakuu ambao wamekuwa wakituelekeze tutunze mazingira,” amesema.
Waziri Jafo amepongeza juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali za kupanda miti ambapo kupitia zoezi la upandaji miti milioni 1. 5 kwa kila halmashauri kwa mwaka limeonesha mafanikio kwa kufikia zaidi ya asilimia 80.
Aidha, Dk.Jafo ameiagiza miti iliyopandwa itunzwe ili isiliwe na ng’ombe huku akitoa siku 14 kwa Stamico kujenga uzio na kuweka geti katika eneo k hilo.
“Dodoma ni mkoa pekee ambao utakuta ng’ombe wanatembea barabarani miti ili mkiipanda isipotunzwa maana yake yote italiwa na ng’ombe Mtendaji Mkuu Stamico nakuagiza ndani ya wiki mbili..
Hata hivyo Waziri Jafo amehimiza matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza kasi ya ukataji wa miti kwa ajii ya kuni na mkaa na hivyo kupunguza changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ambayo husababisha uchumi wa nchi kushuka.
Kwa upande wake Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Doto Biteko,ameitaka STAMICO kuhakikisha wanaisimamia miti hiyo na kuitunza iweze kuishi kwa miaka mingi zaidi.
”Haitakuwa na maana kama tunatumia muda na rasilimali kupanda miti halafu inakufa itakuwa hatutendi haki hivyo tunapaswa kupanda miti mingine.”amesema Dk.Biteko
Waziri Biteko amemshuruku Waziri Jafo kwa kushiriki katika kampeni ya upandaji miti pamoja na kutoa hamasa kwa wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutunza na kuhifadhi mazingira.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema kuwa wanatarajia kupanda miti 10,000 na kwa awamu ya kwanza ilipandwa miti 100 kati ya 2,000 itakayopandwa katika jiji la Dodoma na baadaye 8,000 iliyobaki katika mikoa mingine ambako inaendesha miradi yake.
”Lengo la kampeni hiyo ni kushiriki kikamilifu katika zoezi la utunzaji wa uoto wa asili na kuleta hamasa ya kutunza mazingira ili shughuli za uchimbaji madini ziwe rafiki kwa mazingira.”Dkt.Mwasse
Awali Naye Mkuu wa Mkoa wa Rosemary Senyamule ,ameitaka STAMICO kutafuta teknolojia mbadala wa matumizi ya miti katika shughuli za wachimbaji wadogo wa dhahabu ili kupunguza ukataji wa miti.
”Shughuli za madini ni muhimu na zinapaswa kuwa endelevu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu lakini zinapaswa kuzingatia uhifadhi wa mazingira”amesema
Hata hivyo Senyamule ameahidi kutoa ushirikiano kwa Ofisi ya Makamu wa Rais katika kuifanya Dodoma kuwa ya kijani na kupongeza juhudi zilizofanyika katika kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa.