Na Lucas Raphael,Tabora
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kkkt Dayosisi ya Magharibi Dkt Isaack Laiser amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agasti 23 mwaka huu ili viongozi waweze kuona namna nzuri ya kuwezesha taifa kupanga maendeleo yake
.
Alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua kongamano la sita la vijana wa kanisa hilo kutoka Tanzania bara linalofanyika katika chuo cha utumishi wa umma tawi la Tabora mkoani hapa.
Askofu Dkt Isaack Laiser alisema kwamba wanatanzania wote wanaitajika kujitokea kuunga jitiada za serikali ili kuweza kutambua idadi ya wananchi wake ili iwe rahisi kuweza kupanga maendeleo.
Alisema tukio hilo la kitaifa ambalo linafanyika kila baada ya miaka 10 la kuhesabiwa kwa kujua idadi ya watanzania kwa lengo la kupanga maendeleo kwa watanzania wote.
“Sensa ni jambo la muhimu sana hivyo ni msingi kwa wananchi kujitokeza kuweza kuhesabiwa ili serikali iweze kupanga vizuri maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa” alisema Askofu Dkt Isaack Laiser
Askofu Dkt Isaack Laiser alisema kwamba asitokee mtanzania akupuuza jambo hilo ambalo ni muhimu kwa nchini inayoendeshwa kwa njia ya utawala bora .
“ sensa sio jambo ngeni kwani hata katika historia ya biblia sensa ilifanyika wakati yesu anazaliwa naye alihesabiwa hivyo ni muhimu kwa watanzania kujitokeza kwenda kuhesabiwa “alisema Askofu Dkt Laiser
Hata hivyo askafu huyo aliwataka vijana hao kufanya kazi kwa bidii na kufuata maadili ili kuweza kilijenga taifa kwani Taifa lolote linawatengemea nguvu kazi ya vijana .
Alisema kwamba asilimia 60 ya watanzania ni vijana hivyo muhimu kwao kufanya kazi ya mikono yao kwani bila kufanya kazi kwa bidii taifa litadumaa kimaendeleo.
Alisema kwamba ukisoma katika kitabu cha mithali kuazia mstari wa 10.4” mkono wake mwenye bidii hutajirisha” ndivyo hivyo vijana wanatakiwa kufanya kazi kwa mikono yao ili waweze kufikia mafanikio katika maisha .
Kongamano hilo limehudhuriwa na vijana 700 kutoka dayosisi 27 za Tanzania bara ambalo litarajiwa kumalizika agasti 14 mwaka huu