Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Patrick Golwike akizungumza katika kikao kazi kati ya Wizara hiyo na Wakuu wa Vyuo Binafsi vya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada kilichofanyika jijini Dodoma
Mwakilishi wa Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Lomito Mollel akielezea lengo la kikao kazi kati ya Wizara na Wakuu wa Vyuo Binafsi vya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada kilichofanyika jijini Dodoma
Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo cha Agya Eliseray kilichopo mkoani Tanga Charles Mselema akizungumza katika kikao kazi kati ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Wakuu wa Vyuo Binafsi vya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada kilichofanyika jijini Dodoma
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Grace Chenya akifafanua jambo wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Wakuu wa Vyuo Binafsi vya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada kilichofanyika jijini Dodoma
Baadhi ya wakuu wa Vyuo Binafsi vya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada wakiwa katika kikao kazi kati yao na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuweka utaratibu wa pamoja wa kuwa na mitaala linganifu ya kitaifa ya kozi ya ustawi wa jamii
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Mallum Patrick Golwike katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa Vyuo Binafsi vya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada mara baada ya kufungua kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma Agosti 11, 2022.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
…………………………………………………
Na WMJJWM Dodoma
Serikali imevitaka Vyuo Binafsi vya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada nchini kushirikiana katika kuhakikisha kunakuwa na Mitaala linganifu ya uendeshaji wa kozi ya Ustawi wa Jamii ili kuwa na wataalam wenye umahiri na viwango vinavyohitajika.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma leo Agosti 11, 2022 na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Patrick Golwike wakati wa kikao kazi kati ya Wizara hiyo na Wakuu wa Vyuo Binafsi vya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa ngazi ya Astashahada na Diploma.
Golwike amesema ili kutatua changamoto hizo wizara ilitengeneza Mitaala linganifu ya kitaifa (National Standardized Curricula) pamoja na nyenzo zake za kufundishia kozi ya ustawi wa jamii ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa nchi nzima hivyo eneo pekee lililokuwa limebaki ni kuanzishwa kwa mfumo wa mitihani ya pamoja (Centralized examination system) ili kutahini wanafunzi kwa ubora na viwango sawa.
Ameongeza kwamba baadhi ya changamoto zinazokabili utoaji wa Taaluma hiyo ni pamoja na vyuo kuendesha mafunzo ya kozi hiyo kwa kuiga uzoefu wa mfumo wa Kozi za afya kwa baadhi ya maeneo bila kujali mahitaji ya Mitaala na utofauti wa kada ya ustawi wa jamii na kada ya afya, baadhi ya vyuo kutokuwa na wakufunzi wa kutosha, kuendesha mafunzo kwa kutumia walimu ambao hawana sifa za kufundisha kozi ya ustawi wa jamii kama vile wauguzi, maendeleo ya jamii, walimu wa sekondari kinyume na matakwa ya mitaala pamoja na kutunga mitihani ambayo haina viwango vya kuweza kupima weledi na umahili wa wahitimu.
“Hali hii imeathiri kwa kiwango kikubwa ubora wa mafunzo ya ustawi wa jamii na kutoa rasilimali watu isiyokuwa na weledi na maarifa stahiki hivyo tukiweka utaratibu mzuri tutamaliza changamoto hizi na kuwa na Vyuo vinavyotoa wataalamu mahiri“ alisema Golwike
Aidha alisema Wizara katika kuendelea kutekeleza jukumu lake la kuhakikisha nchi inapata wataalamu wenye weledi na umahiri unaotakiwa, imevikumbusha vyuo kuendesha mafunzo hayo kwa kufuata taratibu na matakwa ya mitaala husika huku Wizara ikiendelea kuandaa utaratibu uliokuwa ukisubiriwa wa kuwa na mitihani ya pamoja ili kupunguza kama siyo kuondoa kabisa mapungufu yaliyojitokeza.
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza katika kikao kazi hicho Mwakilishi wa Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Lomito Mollel alisema lengo la kikao kazi hicho ni kujadili namna ya kusadia uboreshaji wa mitaala ili kuhakikisha taaluma ya ustawi wa jamii itatoa wataalam mahiri na bora.
Naye mmoja wa wakuu wa Vyuo hao kutoka Chuo cha Afya Eliseray kilichopo mkoani Tanga Charles Mselema alisema Vyuo hivyo vitaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha vinatoa wataalamu mahiri na bora wa Ustawi wa Jamii ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa Wataalam hao katika jamii ambao ni chachu ya ustawi na maendeleo ya jamii.