Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa NMB, Isaac Masusu (kushoto) na Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu wa NMB, Straton Chilongola (Kulia) wakiwa wameshikiliza tuzo baada ya kuibuka kinara kwenye Maonesho ya Nane Nane jijini Mbeya
***********************
Benki ya NMB imeibuka kidedea katika taasisi za kibenki na kifedha kwenye maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa mwaka huu mkoani Mbeya.
Mbali na kunyakua tuzo hiyo ya kitaifa, benki hiyo pia iliibuka mshindi katika maonesho ya kanda yaliyofanyika kanda ya Nyanda za Juu, Ziwa na Magharibi, Kaskazini, Mashariki na Kati.
Akizungumza muda mfupi baada ya kupokea cheti cha ushindi, Mkuu wa idara ya Kilimo Biashara wa Benki ya NMB, Isaac Masusu alisema tuzo hizo zinasisitiza dhamira ya benki hiyo kwa kutoa huduma za kibenki na bidhaa zinazoendana na matakwa ya wateja.
Lakini pia, aliongezea kuwa wataendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo na kuwa tayari wameshusha kiwango cha riba mpaka tarakimu moja kwa wateja wake katika sekta ya kilimo.
Maonesho ya Nane Nane yaliyowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo yalizinduliwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango Agosti 1, 2022 na kufungwa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan.