Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akizungumza na waandishiwa habari wakati akieleza Utekelezaji wa shughuli za TET na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akisisitiza jambo wakati akieleza Utekelezaji wa shughuli za TET na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumisshi wa TET wakati akieleza Utekelezaji wa shughuli za TET na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inaendelea kukamilishakazi ya usambazaji wa vitabu vya masomo mbalimbali ngazi ya Sekondari na kukamilisha uandishi wa vitabu vya masomo yote ya Ufundi kidato cha I-IV na masomo ya ziada.
Katika kazi hii Serikali imetenga jumla ya shilingi Bilioni 4,238,569,340 kuwezesha uandishi na uchapaji wa vitabu vya kiada vya masomo haya kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na wasio na mahitaji maalumu kidato cha I-IV.
Ameyasema hayo leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba wakati akieleza Utekelezaji wa shughuli za TET na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Amesema pamoja na kuandaa nakala ngumu za vitabu, TET inatambua na kuzingatia umuhimu wa matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji. Hivyo, vitabu vyote vimewekwa katika mkataba Mtandao inayopatikana katika tovuti ya www.tie.go.tz.
Aidha amesema kwa mwaka wa Fedha 2022/2023, TET inatarajia kuendelea kutoa mafunzo kazini kwa walimu na wasimamizi wengine wa utekelezaji wa mitaala ambapo jumla ya shilingi Bilioni 1,400,000,000 zimetengwa na zimelenga kuwafikia jumla ya walimu na wasimamizi wa utekelezaji wa mitaala 8,500.
Ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali ilitoa shilingi Bilioni 1,243,400,000 kwaajili ya kutoa mafunzo kwa walimu, wathibiti ubora wa shule ambao jukumu lao kubwa ni kufuatilia utekelezaji wa mitaala na wasimamizi wengine wa utekelezaji wa mitaala.
“Kwa kutumia fedha hizi, TET iliweza kutoa mafunzo kazini kwa jumla ya walimu 4,627 wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari. Mchanganuo wa walimu hawa ni; Walimu 200 wa Elimu ya Awali, 2,779 wa Elimu ya Msingi, 927 wa Masomo ya kilimo, Ufundi,Biashara na Sayansi Kimu na 730 wa masomo ya sayansi na Hisabati Ngazi ya Sekondari Kidato cha I-IV”. Ameeleza Dkt.Komba