MKURUGENZI Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.Stephen Elisante,akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni kanda ya kati Jijini Dodoma.
WANANCHI wakiwa katika banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakipata elimu mara baada ya kutembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni kanda ya kati Jijini Dodoma.
AFISA Habari Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.Bathelomeo Wandi,akitoe maelezo zaidi kwa mwananchi aliyetembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni kanda ya kati Jijini Dodoma.
AFISA Elimu Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Titus Mwanzalila,akimueleza mwananchi aliyetembelea banda la Tume hiyo hatua zinafanyika kwa wananchi anapotaka kupata kitambulisho katika Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni kanda ya kati Jijini Dodoma.
MKURUGENZI Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.Stephen Elisante,akizungumza na waandishi wa habari katika banda la tume hiyo katika Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni kanda ya kati Jijini Dodoma.
……………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
MKURUGENZI Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.Stephen Elisante amesema kuwa wanatumia maonesho ya Nanenane kufanya maandalizi ya uchaguzi kwa kutoa elimu kwa mpiga kura kwa wananchi wanaotembelea banda lao.
Hayo ameyasema leo Agosti 7,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la tume hiyo katika Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni kanda ya kati Jijini Dodoma.
Ambapo amebainisha kuwa wao kama tume kila wanapopata na fursa ya kukutana na wananchi basi hutumia muda huo ipasavyo kuwaelimisha kuhusu masuala ya uchaguzi hivyo kuwepo kwa banda hilo katika viwanja hivyo ni fursa tosha kwa kila mwananchi kufika na kupata elimu kwa mpiga kura.
Bw.Stephen amesema kuwa kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo uchaguzi mkuu unafaanyika kila baada ya miaka mitano hivyo kila baada ya uchaguzi tume inaanza rasmi maandalizi ya uchaguzi unaofuata kwa kutoa elimu kwa wapiga kura.
“Tume ipo kazini kwa maandalizi ya uchaguzi unaofuata na moja ya maandalizi hayo ni kutoa elimu kwa mpiga kura sasa hapa kwenye banda letu tumekuja na baadhi ya vifaa ambavyo huwa vinatumika kipindi cha uchaguzi kama vile mfano karatasi za kura,fomu mbalimbali za matokeo,fomu zinazotumika wakati wa uboreshaji,masanduku ya kura,mashine ya BVR,Majalada ya nukta nundu kwa ajili ya wapiga kura wenye uono hafifu na vitabu mbalimbali vinavyohusiana na uchaguzi”Amesema Bw.Stephen
Pia amewapongeza wananchi ambao tayari wameshapata elimu ya mpiga kura katika banda hilo na kuongeza kuwa wapo tayari kuendelea kutoa elimu hivyo akawataka wananchi wanaotembelea maonesho hayo kuhakikisha wanatembelea banda la tume ya taifa ya uchaguzi ili kupata elimu mbalimbali itakayowasaidia kufahamu zaidi juu ya uchaguzi