Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Mbarak Alhaji Batenga akipata maelezo ya ufugaji bora wa kuku kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Charity Farm ,Jonas Kalokola katika maonyesho ya nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Themi Njiro
Moja ya Banda la kuku ambalo linatengenezwa na kampuni hiyo Kwa ajili ya kufugia kukua kwa njia salama.
Mkurugenzi wa kampuni ya Charity Farm ,Jonas Kalokola (mwenye kofia nyeupe) akimuonyesha Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Mbarak Alhaji Batenga moja ya Banda la kuku linalotengenezwa na kampuni hiyo.
………………………………………
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Zaidi ya wananchi Laki moja wanatarajiwa kufikiwa na elimu juu ya ufugaji bora wa kuku na kuondokana na ufugaji wa kimazoea na kuweza kufuga kibiashara.
.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi wa mabanda ya kuku na utoaji elimu juu ya ufugaji bora ya Charity Farm ,Jonas Kalokola wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya huduma hiyo katika viwanja vya nanenane vilivyopo Themi Njiro.
Kalokola amesema kuwa,elimu hiyo inatarajiwa kutolewa kwa wafugaji hao katika maonyesho hayo ili waweze kufuga kisasa zaidi na kuondokana na changamoto mbalimbali na hatimaye kuweza kupata soko la uhakika na kujikwamua kiuchumi.
“Watu wengi wamekuwa wakifuga kuku ila hawana mbinu bora za kisasa juu ya ufugaji wa kuku na kuweza kufuga kibiashara kwa ajili ya kupata masoko ndani na nje ya nchi kwani soko la kuku ni kubwa na wafugaji wengi hawana mbinu bora za ufugaji huo.”amesema.
Aidha ameongeza kuwa,tangu maonyesho hayo yameanza idadi kubwa ya wakulima imeweza kufikiwa na elimu hiyo ambayo wengi wao walikuwa hawana ambapo mwisho wa maonyesho hayo wanatarajia kuona matokeo tofauti ya ufugaji huo wa kisasa kwa wakulima hao na kuweza kupata soko la uhakika.
Kalokola amesema kuwa, kampuni hiyo ina miaka minne Sasa ambapo mbali.na kutoa elimu hiyo imekuwa ikiuza vifaranga, ujenzi wa cage za kisasa,ujenzi wa local cages,ujenzi wa mabanda ya kuku,kufunga system za maji,na kutoa ushauri wa ufugaji wa kisasa na kuweza kupata masomo ya uhakika ndani na nje ya nchi.
Aidha aliwataka wananchi kufika katika Banda hilo ili waweze kupata elimu ya kutosha juu ya ufugaji huo na kuweza kufuga kibiashara na kupata masoko ya uhakika.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mbarak Alhaji Batenga akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo,alipongeza kampuni hiyo kwa namna ambavyo inatoa elimu kwa wafugaji wa kuku juu ya ufugaji bora wa kisasa ambao utawawezesha kufuga kisasa na kuweza kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.
Batenga amesema kuwa, wananchi wanapaswa kutambua kuwa maonyesho ya nanenane ni shule ya bure ambayo inamlenga kila mwananchi kuweza kufika na kuweza kujifunza maswala mbalimbali na kuweza kujikwamua kiuchumi.
“Nitoe rai kwa wananchi kutembelea mabanda mbalimbali kujionea shughuli mbalimbali zinazoonyeshwa huko na kuweza kupata elimu ambayo wakiitumia kwa vitendo wataweza kujikwamua kiuchumi na hatimaye kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.”amesema.