Makamu Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,
ameshiri pamoja na wana CCM wa Kata ya Oysterbay kuwachagua viongozi
wapya wa Chama katika kata hiyo.
Uchaguzi huo umefanyika leo
Agosti 6, 2022 katika Shule ya Msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam
ambapo viongozi mbalimbali wamechaguliwa.
Akiwasalimia wana CCM
wenzake baada ya upigaji kura, Kinana amesema Chama kinafurahishwa na
mwitikio mkubwa wa wanachama kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali na
kufanya uchaguzi kwa amani.
Kinana amesema hadi sasa mwenendo wa u
haguzi unakwenda vizuri na kwamba changamoto chache zinazojitokeza
hususani kuhusu malalamiko ya ukiukwaji wa haki, hatua zitachukuliwa na
haki itatendeka.
“Yapo malalamiko ya hapa na pale, lakini nina
hakika yatafanyiwa kazi ili mwanachama akishinda ashinde kwa haki.
Msingi wa Chama hiki ni kutenda haki, kwa hiyo nina hakika viongozi
watatenda haki,” amesema Kinana.
Nafasi zilizopigiwa kura ni
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Oysterbay, wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa,
wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya na wajumbe wa halmashauri kuu ya kata
hiyo.