Na Prisca Libaga Maelezo Arusha
KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha,Missaile Albano Mussa amesema kuwa amekuja Arusha kuendeleza majukumu ya serikali ya awamu ya sita sanjari na ilani ya ccm hivyo akaomba ushirikiano kutoka kwa watumishi wa serikali ili awaze kutekeleza ipasavyo majukumu yaliyopo.
.
Ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika jengo la Mkuu wa Mkoa na kusisitiza ushirikiano kwa watumishi wengine wa serikali ili kutimiza majukumu yaliyopo mbele yao na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mwezi uliopita Rais Samia Suluhu Hassani,amefanya mabadiliko ya baadhi ya wakuu wa Mikoa na Makatibu tawala,ambapo alimuondoa aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kihamia na nafasi yake kuchukuliwa na Mussa ambae amehamia kutoka Mkoa wa Songwe
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Abeli Ntupwa amempongeza aliyekuwa katibu tawala wa mkoa huo Dkt Athumani Kihamia,kwa utendaji wake uliotukuka ambao umeacha alama isiyofutika ambayo wataitumia kama mwongozo.
Ntupwa ambae pia ni Katibu Tawala Msaidizi,elimu,Sekretariet ya mkoa,ameeleza kuwa Dkt Kihamia alikuwa kiongozi mwelekezaji,aliimarisha system ya utendaji ambayo wataendelea kuifanyia kazi kwa kuwa ina mafanikio makubwa kwenye utumishi wa umma.
Amesema walikuwa wakifanyia kazi maelekezo kwa haraka na sasa kasi hiyo ya uwajibikaji wataitumia kutekeleza maelekezo ya uwajibika kwa Katibu Tawala Mussa
Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Afya kwenye sekretariet ya mkoa, Dkt Silvia Mamkwe,amesema kuwa Dkt Kihamia amewajengea timuwork kwa kufanyakazi kwa pamoja ,alikuwa mwelekezaji na mshauri,aliwajali watumishi wa ngazi za chini wakiwemo wenye ulemavu
Mamkwe,ambae ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha,amesema kuwa mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja umeongeza ufanisi na kuwepo ubunifu mambo ambayo yamechangia uboreshaji wa utendaji na kuongeza kuwa shughili za Umma ni kupokezana vijiti
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Utawala na Rasilimali watu ya Mkoa, David Lyamongi, amesema Kihamia alikuwa ni kiungo mzuri sana aliimarisha mawasiliano ya haraka kwa kasi kubwa katika halmashauri zote saba za mkoa huo hivyo watamkumbuka
Amesema kuwa Dkt,Kihamia, alisisitiza watumishi kufanya kazi kwa viwango alisimamia na kuelekeza masuala ya utumishi ikiwemo watumishi kulipwa saa za ziada kunapokuwepo kazi za dharura.
“Dkt. Kihamia ni mtu aliyejali watumishi wa ngazi za chini zaidi hasa katika kupata Stahiki zao, hivyo wataliendeleza, hilo katika kukuza ufanisi wa watumishi”. amesisitiza Lyamongi
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli, Raphael Siumbu,kwa niaba ya wakurugenzi wa halmashauri zingine za mkoa huo, amesema kuwa Dkt Kihamia alikuwa kiongozi mwadilifu,hivyo watatoa ushirikiano kwa katibu tawala mpya.
Akiwaaga watumishi wa Sekretariet ya mkoa Dkt Kihamia amesema Kuwa amekuwepo Arusha kwa kipindi cha miezi 14.
Amesema kuwa mwaka wa fedha 2021/2022 mkoa ulipokea shilingi bilioni 1.3, kwa ajili ya shughuli za maendele za ujenzi, ukarabati Jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa,ukarabati nyumba ya mkuu wa wilaya ya Arusha, sanjari na ujenzi wa ukuta wake wa uzio ukarabati ofisi ya mkuu wa wilaya ya Longido ,uchimbaji kisima kirefu cha maji ,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Amesema kuwa ukarabati ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ujenzi ,ukarabati choo cha ofisi ya mkuu wa wilaya ukarabati wa nyumba ya Katibu Tawala Mkoa ukarabati nyumba ya Mkuu wa Mkoa, ukarabati wa ofisi mbilii za tarafa .n.k