Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mragili, amezitaka shule za
msingi na sekondari wikayani hapa kujipanga kuingia katika mfumo wa ufundishaji
kwa njia ya kidigitali kwa kuwa mpango wa serikali ni kutaka utendaji wote uwe unafanyika kidigitali.
Alisema hayo jana baada ya kukabidhi walimu vishikwambi 270 ambavyo
vitatumika katika shule 135 za msingi na sekondaji kwa ajili ya kufundisha
masuala ya elimu ya uzazi na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya
ukimwi.
“Mpango wa serikali ni kutaka kuhama kabisa katika utendaji wa
‘analog’ kwenda kwenye utendaji wa kidigitali hivyo lazima shule zijipange
kuingia katika mfumo huo,” alisema.
Mragili alisema anafahamu zipo shule zitakuwa ndio zinaanza kwa mara ya
kwanza matumizi ya kidigitali katika ufundishaji hivyo ziwe mfano bora kwa
zingine ili ziweze kuvutika kutumia teknolojia hiyo.
“Wengi wetu hapa mna simu za smartphone mnazitumia vizuri sasa
kinachofanyika hapa umeongezewa ukubwa wa ‘screen’ tu kinachofanyika katika
vishikwambi hivi ni sawa na simu tu ziadi hapa kilichongezewa ni programu
maalum ya masomo haya,” alisema.
Mragili alisema shule ambazo zimebahatika kupata vishikwambi hivyo ziwe
mfano kutumia vifaa hivyo ili kuzivutia zingine kutumia teknolojia hiyo na
shule zione umuhimu wa kuongeza vishikwambi zaidi kwani viwili ambavyo
vimetolewa kwa kila shule havitoshelezi.
Alisema walimu lazima watambue kuwa mpango huu ulipoanzisha tayari tafiti
ziliehafanyika na kuona kuna tatizo la elimu ya uzazi kwa vijana hivyo
wahakikishe wanafundishwa ili waweze kujitambua na kupunguza maambukizi ya VVU.
“Naomba Singida tuwe miongoni mwa halmashauri zitakazofanya vizuri
katika proramu hii ili kuwafanya vijana wawe na afya njema na wafikie ndoto zao
katika maisha yao,” alisema.
Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza suala la itunzaji wa vishikwambi hivyo ili
visaidie vijana wengine zaidi na kwamba kuvifabya kuwa mali ya shule sio kwamba
utunzani uwe wa kulegalega.
Aidha, aliishukru serikali kwa kutoa vishikwambi kwa kutoonyesha ubaguzj
ambapo vimetolewa kwa shule za serikali na binafsi kwa suala la elimu ya afya
huwezi kubagua kati ya wanafunzi wanaosoma shule binafsi na za serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula,
alisema vishikwambi hivyo vitatolewa kwa walimu 270 waliopewa mafunzo ya namna
ya kuvitumia na vitakuwa mali ya shule.
Alisema halmashauri yake imekuwa miongoni mwa Halmashauri 20 kati ya 184
zilizogawiwa vishikwambi hivyo ambapo shule za msingi 94 na sekondari 41 ndizo
wanafunzi wake watafundishwa masomo ya uzazi wa mpango na jinsi ya kujikinga na
maambukizi ya VVU.
Alisema serikali imetoa vishikwambi hivyo ili kuweza kutoa elimu ya uzazi
wa mpango na maambukizi ya VVU ili kufikia malengo ya mradi unaojulikana kama
Timiza Malengo unaoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Chaula alitoa wito kwa walimu pamoja na kwamba vishikwambi vimetolewa kwa
ajili ya kufundishia masualanya elimu ya uzazi lakini pia vitaweza kutumika
kufundisha masomo mengine kwasababu vina uwezo wa kuhifadhi ‘materials’ ya
masomo mengine yanayofindishwa shuleni.
Alisema mwelekeo wa serikali ni kufanya kila kitu kufanyika kwa njia ya
kidigitali ambapo kutumia teknolojia hii kutapunguza matumizi ya karatasi na
wanafunzi watafundishwa elimu ya uzazi na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya
VVU kwa njia ya picha.