Mkuu wa Wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo wa kushoto akikagua bidhaa mbali mbali katika Banda la Wilaya ya Mafia kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Martine Ntemo.
**************************
Na Victor Masangu
Maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nanenane 2022) kwa Kanda ya Mashariki yanaendelea Mkoani Morogoro kwa kishindo kwa kushirkisha mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga na Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yenye Kauli Mbinu isemayo ‘Ajenda 10/30 Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mpango Bora wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi’, yameendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi kama sehemu ya kujifunza mbinu mbali mbali za kisasa za kilimo na ufugaj
Katika maonyesho hayo ambayo yanazidi kushika kasi zaidi pia yametembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Ghaibu Lingo ambaye alitembelea mabanda mbali mbali likiwemo banda la Wilaya ya Mafia ambapo amejionea bidhaa mbali mbali.
Akiwa katika banda la Mafia amejionea namna huduma zinavyotolewa katika banda hilo ambapo amepongeza jinsi mazao katika vipando yalivyostawi na hivyo kuweza kutoa taswira halisi ya faida za kuwepo kwa maadhimisho haya kama sehemu ya mafuzo kwa vitendo.
Aidha, kwa upande wa zao la mwani, Mhe. Lingo alisisitiza kuimarishwa kwa usimamizi zaidi na uendelezaji wa zao hilo kwani linaweza kuwa mkombozi mkubwa wa kiuchumi kwa wananchi wa maeneo ya pwani na visiwani.
Katika maonyesho hayoBanda la Kisiwa cha Mafia limesheheni bidhaa za samaki, dagaa, nazi, korosho na mwani ambazo ubora wake ni wa kipekee na zina umaarufu mpaka nchi za jirani.