Mkurugenzi Mtendaji wa Mkombozi Commercial Bank Plc Bw. Respige Kimati (kulia) akikabidhi kitabu cha ajenda ya Mkutano Mkuu 13 wa Wanahisa wa benki hiyo kwa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dodoma la Kanika Katoliki, Beatus Kinyaiya (kushoto) ambaye ni mkurugenzi wa bodi ya Mkombozi wakati wa mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank Plc, Bw. Gasper Njuu
*************************
Benki ya Biahara Mkombozi imepatapata faida baada ya kodi ya kiasi cha shilingi bilioni 3.0 kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Desemba 2021 jambo ambalo lilitokana na ufanisi wa kiutendaji wa biashara na matokeo chanya ya utekelezaji mikakati mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa wanahisa, Mwenyeki Mpya wa Bodi ya wakurgenzi Bw.Gasper Njuu alisema Benki ilipata matokeo ya kuridhisha katika vigezo muhimu vya mizania ya viwango vya upatikanaji wa faida.
Alisema, Benki ilipata faida ya kuvutia na ubora katika ujenzi wa mtaji uliochangiwa na ufanisi wa kiutendaji wa biashara na matokeo chanya ya utekelezaji mikakati mbalimbali ya maendeleo. Tulijikita katika fursa za ukuaji wakati tukichukua hatua chanya kukabiliana na changamoto zilizokuwa katika mazingira yetu ya kiutendaji.
Bw. Njuu aliongeza kwamba licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza mwaka 2021, Benki inaendelea kujikita kimkakati kupanua mawasiliano ya Benki na wateja kupitia huduma za mawakala, na vituo vidogo vya huduma za kibenki chini ya matawi.
Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya Mkombozi Mkurugenzi Mtendaji Bw. Respige Kimati alisema, Utendaji wetu katika mwaka huu umetuweka katika hali njema ukilinganisha na mwaka uliotangulia (2020) katika viwango vya msingi, hususan kimtaji na utekelezaji wa hatua za kimkakati.
Akihutubia kwa zaidi ya wanahisa 500 waliohudhuria mkutano huo Bw. Kimati alisema, Matarajio yetu ya maendeleo ya biashara na ukuaji yanahitaji mtaji endelevu, hususani kwa kuingiza mtaji mpya ili kusaidia uwekezaji muhimu na ukuaji wa
mizania. Wito wetu kwa wanahisa ni kuendelea kuunga mkono mipango ya uwekezaji ya Benki katika azma hii ili kutoa matokeo yenye faida, thabiti na endelevu kwa Benki. Baada ya kupita awamu ya miaka mitatu ya mabadiliko ya biashara na kujipanga
upya, Menejimenti na Bodi inaandaa mpango mkakati wa muda wa kati ambao utatumiwa kama dira ya kuendeleza Benki yetu ili kufikia malengo yake
Wanahisa walikuwa na jambo la kufurahia pale ambapo Bw. Kimati alitangaza kuwa benki iliongeza fedha za wanahisa kwa asilimia 26 hadi kufikia shilingi bilioni 25.82 kutoka shilingi bilioni 20.57 za mwaka uliotangulia. Ukuaji huu ulichangiwa na kuingizwa kwa mtaji nyongeza wa shilingi bilioni 2.2 na faida ya mwaka iliyowekezwa.
Aliendelea kwa kusema kwamba, Uwiano wa mtaji ulikuwa Shilingi Milioni 19,589 wenye mnyambulisho wa asilimia 14.63 na 14.63 ukilinganishwa na uwiano wa mtaji wa shilingi millioni 16,423 wenye unyambulisho wa asilimia 11.08 na 11.08 kwa mwaka 2020. Mtaji wa Benki upo juu ya mtaji unaotakiwa kisheria wa Shilingi Bilioni 15.
Akizungumzia mpango mkakati wa mwaka 2022 hadi 2023, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Gasper Njuu, alisema wana mpango wa kufanya biashara kidijitali kama vile utumiaji wa mawakala, malipo kwa njia ya mitandao ya simu, matumizi ya mitandao katika miamala ya kibenki na hatua madhubuti za usimamizi wa fedha.
“Tunataka pia kupanua mawasiliano ya benki na wateja kupitia huduma za mawakala na vituo vidogo vya huduma za kibenki chini ya matawi ambapo tayari tumesajili mawakala 140 kati ya 250 waliokukusudiwa kwa mwaka 2022, tumezindua huduma ya ukusanyaji wa ada mbalimbali za Makanisa (SADAKA Digital) ambapo tumefanikiwa kusajili jumla ya Parokia 40 Dsm pekee katika hatua za awali kati Parokia 250 kwa nchi nzima kwa mwaka 2022, alisema.
Mwenyekiti wa Bodi Bw. Njuu alisema Mkombozi Benki itaendelea kuimarisha ubunifu na uwekezaji katika teknolojia ili kutoa huduma na kuboresha sifa njema kutoka kwa wateja (uwekezaji katika mfumo mpya wa kibenki wa msingi).
Kwa upande wake, Mhe Baba Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Mkombozi Benki alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji Bw. Respige Kimati kwa ufanisi katika utendaji tangu ashike nafasi hiyo, kwani alikuta Benki ikiwa na mtaji wa shillingi billioni 8 ambao ni chini ya mtaji unaotakiwa kisheria na kuupandisha mpaka kufikia mtaji wa shilling billioni 19.9 mwaka wa 2021.
“Huu ulikuwa wakati mkubwa wa mabadiliko ya Benki kwani kiwango cha chini cha mtaji wa mabenki kisheria ni shillingi billioni 15 na ndani ya miaka miwili Bw. Kimati aliweza kupandisha Mtaji wa Benki kuwa juu ya mtaji unaotakiwa kisheria. Unastahili pongezi sana na haya ndio masuala ambayo wanahisa wanataka kusikia,” alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashaya ya Mkombozi, Bw. Gasper Njuu akielezea jambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wanahisa wakifuatilia mkutano huo katika ukumbi wa Ubungo Plaza.