Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Techno Auditors, Lupiana Michael akizungumzia bonanza la michezo la timu za veterans ambazo zitachuana Jumapili (Julai 31) kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Techno Auditors, Lupiana Michael (kulia) akiangalia uwanja wa Kijitonyama (Bora) ambao utakaotumiwa na timu za saba za maveterans katika bonanza maalum lililopangwa kufanyika Jumapili (Julai 31, 2022). Pembeni ni mshauri wa masuala ya kodi wa taasisi ya Techno Auditors Richard Mabeba.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Techno Auditors, Lupiana Michael (kulia) akiwa katika majadiliano na katibu mkuu wa timuya Kijitonyama Veterans Amon Petro (Kiki) (katikati) na mshauri wa masuala ya kodi ya taasisi ya Techno Auditors, Richard Mabeba.
…………………………….
Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
Jumla timu saba za maveterans zitashiriki katika bonanza maalum la mpira wa miguu litakalofanyika kesho Jumapili (Julai 31, 2022) kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama.
Bonanza hilo limeandaliwa na taasisi ya ukaguzi wa mahesabu, ushauri wa kifedha, biashara na masuala ya kodi ya Techno Auditors kwa kushirikiana na timu ya Kijitonyama veterans.
Mkurugenzi mtendaji wa Techno Auditors, Lupiana Michael alisema kuwa mbali ya kuhamasisha maendeleo ya michezo, bonanza hilo litakuwa maalumu la kuadhimisha au kusheherekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa taasisi yao.
Lupiana alizitaja timu hizo kuwa ni Tanga Veterans, Tabora Veterans, Goba Veterans, Uganda Veterans, Kijitonyama Veterans, Posta Veterans and Techno Auditors veterans.
Aifafanua kuwa kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili ambazo zitatolewa na waandaaji.