***********************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ameagiza viongozi wa kata ya Kikongo kushughulikia changamoto za migogoro ya ardhi na kusisitiza endapo atabaini kuna mtu mbabaishaji basi atashughulika nae.
Alitoa agizo Hilo wakati wa ziara ya kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Kikongo na kusikiliza changamoto iliyopo ya migogoro ya ardhi kati ya wawekezaji na wanachi wa kata hiyo
Alieleza kuwa,kats hiyo inadaiwa kuwa na changamoto na migogoro ya ardhi suala ambalo linapaswa kutafutiwa ufumbuzi.
Aidha ,ameagiza shamba ambalo halina mgogoro shamba namba 30/1 liendelezwe “kuna mashamba mawili moja lina mgogoro na lingine halina mgogoro kwanini ambalo halina mgogoro lisiendelezwe.”
alisema Kunenga.
Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza viongozi washughulikie haraka shamba lenye mgogoro ili wawekezaji waendelee na shughuli Yao.
“Baadhi ya viongozi acheni ubabaishaji,na nahimiza, suala la haki !!!”Mwenye haki apewe ama mwananchi ana haki apewe haki yake na kama muekezaji ana haki apewe haki yake.” alieleza Kunenge.
Vilevile,Ofisa Ardhi Grayson Gipson aliombwa kutoa mrejesho uliotolewa kipindi cha Waziri wa nyumba , Maendeleo na Makazi William Lukuvi kwenye ziara yake aliyofanya Julai 2021, ambapo alielekeza kuhusu mashamba mawili yanayomilikiwa na Trans continental, la Kwanza ni 30/1 na la pili ni 30/2.
Ofisa ardhi huyo, alieleza kuwa shamba namba 30/1 halina changamoto hivyo kampuni ipo tayari kwa kufanya vipimo na kushughulikia shamba namba 30/1.
Alisema, shamba namba 30/2 lina changamoto na kampuni ipo tayari kushughulikia shamba namba moja tu ambalo halina mgogoro.