Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe. Donald Wright, Mkurugenzi wa Shirika la kudhibiti na kukinga magojwa (US Centers for Disease Centrol and Prevention – CDC), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ugonjwa wa Uviko – 19 kwa watumishi wa Afya (Extension of Community Health and Care Outreach – ECHO) leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kimeanzishwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la CDC.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wataalam wa afya wanaoendesha kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ugonjwa wa Uviko – 19 kwa watumishi wa afya wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho uliofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la kudhibiti na kukinga magojwa ya (US Centers for Disease Centrol and Prevention – CDC), Dkt. Rochelle Walensky akiipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza kudhibiti magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Uviko-19 wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ugonjwa wa Uviko – 19 kwa watumishi wa Afya (Extension of Community Health and Care Outreach – ECHO) uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam..
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ugonjwa wa Uviko – 19 kwa watumishi wa Afya (Extension of Community Health and Care Outreach – ECHO) leo katika Hospitali hiyo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalam mbalimbali wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Uviko – 19 wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ugonjwa wa Uviko – 19 kwa watumishi wa Afya (Extension of Community Health and Care Outreach – ECHO) uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe. Donald Wright, na viongozi mbalimbali baada ya uzinduzi wa wa Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ugonjwa wa Uviko – 19 kwa watumishi wa Afya (Extension of Community Health and Care Outreach – ECHO) uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Khamisi Mussa
…………………………………..
Na: Genofeva Matemu – Dar es Salaam
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeipongeza Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Kudhibiti na Kukinga magonjwa la nchini Marekani (US Centers for Disease Control and Prevention – CDC) kushirikiana na Tanzania kuboresha huduma za afya na kufungua Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kwa watumishi wa afya kuhusu ugonjwa wa Uviko 19 (Extension of Community Health and Care Outreach – ECHO).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Kituo hicho kitakua kinatumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya nchi nzima kuhusu masuala mbalimbali ya ugonjwa wa Uviko – 19 ikiwemo jinsi ya kudhibiti maambukizi, namna ya kumhudumia mgonjwa wa Uviko – 19 na namna ya kufanya vipimo vya ugonjwa huo.
“Tumefungua kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kwa watumishi wa afya kuhusu ugonjwa wa Uviko 19 kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani kupitia shirika la Kudhibiti na kukinga magonjwa la nchini Marekani (US Centers for Disease Control and Prevention – CDC) pamoja na Taasisi ya Management and Development for Health – MDH inayofanya kazi na CDC”,
“Kwaniaba ya Serikali tunawashukuru sana shirika la Kudhibiti na kukinga magonjwa la nchini Marekani (US Centers for Disease Control and Prevention – CDC) kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa tunadhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini Tanzania ikiwemo ugonjwa wa Uviko – 19”, alisema Mhe. Ummy
Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa Shirika la Kudhibiti na Kukinga magonjwa la nchini Marekani (US Centers for Disease Control and Prevention – CDC) limekua na utayari katika kusaidia programu mbalimbali za afya hapa nchini ikiwemo ugonjwa wa HIV, Kifua Kikuu (TB), Malaria, Uviko – 19, chanjo ya Uviko – 19 pamoja na kuboresha mfumo wa afya nchini.
“Hadi kufika jana Julai 25, 2022 Tanzania tumefanikiwa kutoa chanjo ya Uviko – 19 kwa watanzania milioni 12.8 ambayo ni sawa na asilimia 41.8 tukiwa ni lengo la kifikia asilimia 70 ya Watanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea hii ni kutokana na ushirikiano tunaoupata kutoka katika Shirika hili la CDC”,
“Hadi sasa tuna vituo vikubwa 8 nchini ambavyo vinauwezo wa kutoa elimu dhidi ya ugonjwa wa Uviko – 19, vituo vidogo vipo 272 na kuna vituo 89 ambavyo wadau mbalimbali wanaendelea kuvifungua yote hii ni kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Uviko – 19”, alisema Waziri Ummy
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Faraja Chiwanga amesema kuwa kituo hicho ni kikubwa hapa nchini ambacho kitakua kinatoa elimu kwa njia ya mtandao kwa watumishi wa afya kuhusu ugonjwa wa Uviko 19 lengo ikiwa ni kuwafikia watumishi wa afya wengi katika maeneo yote nchini hasa maeneo ya pembezoni mwa nchi.
“Tutahakikisha kuwa watumishi wote wanapata uelewa sahihi wa jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa Uviko – 19 kama ambavyo tunafahamu yakuwa ugonjwa huu upo na tutaendelea kukaa nao hivyo kuhakikisha kuwa kiwango kile kile cha huduma kinachotolewa katika vituo vikubwa kiweze kutolewa hata katika vituo vidogo vya afya hapa nchini”,
“Ni ngumu kuwa na wataalam mabingwa katika maeneo yote nchini ndio maana tumeona umuhimu wa kuanzisha mafunzo haya ili wale wataalam mabingwa watakaokuwa wanafuatilia miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya kupitia mafunzo haya kwa njia ya mtandao waweze kubadilishana uzoefu na wataalam wenzao”, alisema Dkt. Faraja
Aidha Dkt. Faraja amewaomba wataalam wa afya walioko katika vituo vidogo vya afya nchini kujitokeza kuelezea changamoto walizonazo katika utoaji huduma kwa wagonjwa wa Uviko – 19 ili kupitia programu hiyo waweze kupatiwa msaada wa jinsi wa kutatua changamoto zao na kuwahudumia wagonjwa hao kiusahihi.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Kudhibiti na Kukinga magonjwa la nchini Marekani (US Centers for Disease Control and Prevention – CDC) Dkt. Rochelle Walensky amesema kuwa CDC imeshirikiana na Serikali ya Tanzania kuanzisha mafunzo hayo ili elimu sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa Uviko – 19 iweze kwenda hadi kwa wananchi waliopo maeneo yote nchini hivyo kupunguza kusambaa kwa ugonjwa huo.
“Wataalamu hawa mabingwa mliowaandaa hapa kwa ajili ya elimu ya Uviko – 19 na namna ya kujikinga na ugonjwa huu watakua walimu wazuri kwa wataalam wenzao wa afya waliopo katika vituo vidogo nao kupitia elimu hiyo wataweza kupeleka utaalam huo kwa wananchi wanaowazunguka hivyo kidhibiti ugonjwa wa Uviko – 19”, alisema Dkt. Walensky