Kaimu Katibu tawala mkoa wa Arusha, Abel Mtupwa akizungumza katika hafla hiyo jijini Arusha leo.
Msemaji wa Taasisi hiyo ,Shehe Haruna Hussein akizungumza katika hafla hiyo jijini Arusha leo
Viongozi wa dini pamoja na viongozi wa mila wakiwa katika mkutano huo uliofanyika jijini Arusha Leo
**********************
Julieth Laizer,Arusha
Arusha.Viongozi wa dini pamoja na wazee wa kimila (Malaigwanan) wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kushiriki katika zoezi la kuhesabiwa huku akiwataka kutoweka imani tofauti katika zoezi hilo.
Hayo yamesemwa Leo julai 27 jijini Arusha na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Abel Mtupwa wakati akizungumza katika semina ya viongozi wa dini na mila mkoa wa Arusha iliyoandaliwa na Taasisi TWARIQATUL QADIRIYA JAILANIYA ARRAZAQIYA Tanzania .
Mtupwa amesema kuwa,ni wajibu wa kila kiongozi kushirikiana kwa pamoja kila mmoja kwa nafasi yake ili watu waweze kushiriki kwa wingi katika zoezi la sensa ili waweze kupata huduma stahiki kwani wasipohesabiwa Serikali itashindwa kupanga mipango ya bajeti ya maendeleo .
“Nawaombeni sana katika zoezi hili tusiweke imani tofauti zaidi bali tufanye kwa umoja wetu ,utamaduni,na uzalendo wa Taifa ketu la Tanzania ili watanzania waweze kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa na kuweza kuirahisishia kazi Serikali katika bajeti zake “amesema.
Kwa upande wa Msemaji wa Taasisi hiyo nchini,Shehe Haruna Hussein amesema kuwa,wao kama taasisi wamekuwa wakiunga mkono shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan ikiwemo zoezi hilo la sensa .
Haruna amesema kuwa,zoezi la sensa ya watu na makazi ni kwa maslahi ya nchi yetu,na kila mmoja kwa nafasi yake ajitolee katika kuhamasisha bila kutegemea malipo yoyote ,bali wajitolee kufanikisha swala hilo kila mmoja kwa imani yake
“swala la sensa ni muhimu sana kwa jamii yetu na kila mmoja ahakikishe anaiunga Serikali mkono kwa kuhamasisha zoezi hilo ili liweze kufanyika kwa umakini na kuirahisishia kazi Serikali katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.”amesema Shehe Haruna.
Naye Mshili Mkuu wa kabila la wameru ,Esrona Sumari amesema kuwa, ameihakikishia serikali kuwa zoezi la sensa litafanyika kwa amani na watanzania watajitokeza kwa wingi kwani wao kama viongozi wa dini wapo bega kwa bega kuunga mkono zoezi hilo.
Kiongozi wa mila kabila la wamasai(Laigwanani ),Olekisongo Meijoo amesema kuwa,akiwa kama kiongozi wa kimila atahakikisha wananchi wa jamii hiyo wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo hasa katika kipindi hiki ambacho Rais Samia anapambana kuiepeleka nchi mbele katika swala zima la maendeleo ya nchi.