*****************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge ,amewataka wananchi wa kata ya Mbwawa kutafuta eneo jengine la kujenga kituo cha Afya kutokana na eneo la Kwanza kutokidhi vigezo na masharti ya serikali .
Aidha ametoa maelekezo kuwa kituo cha Afya Cha awali kifanyie marekebisho kwa kujenga wodi ya wazazi.
Kunenge pia ameagiza wananchi hao kutumia fedha walizouza trekta Shillingi milion 9 kuanza ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati hiyo.
Agizo hilo amelitoa ,wakati wa mkutano wa wananchi wa kata hiyo badala ya kutokea mgogoro wa ardhi katika eneo la ujenzi wa kituo hicho.
Kunenge amewaeleza wakazi wa Mbwawa ,kuwa eneo lao walilochagua ambalo lina ukubwa wa hekari 6 ambazo ni ndogo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya, kuwa kwa mujibu wa katiba ya nchi kituo cha Afya kinatakiwa kuwa na hekari 15.
“Utaratibu wa kujenga kituo cha Afya ni lazima eneo liwe na ukubwa wa hekari 15 “sasa eneo hili no hekari 6 tu hivyo halitoshi badala yake nataka eneo hili mjenge wodi ya wazazi” alisema kunenga.
Amewaeleza ,wananchi wa Mbwawa kutumia eneo hilo kwaajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi na amewaruhusu kutumia fedha hizo Shilingi milioni tisa kuanza ujenzi wa wodi ya wazazi na kusema serikali ya Mkoa kupitia Halmashauri itasaidia kumalizia ujenzi huo.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha ,Sara Msafiri alimueleza Mkuu wa mkoa kuwa eneo hilo la Mbwawa linahitaji kuwa na kituo cha Afya Kwan ni eneo lenye wananchi wengi na wanapata changamoto ya kufuata huduma za Afya katika kituo cha Mlandizi
Sara alieleza kuwa walishafanya utaratibu wa kutafuta eneo lingine la kujenga kituo cha Afya, badala ya eneo la awali kutokukidhi vigezo.
Aliendelea kusema tayari serikari ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mama Samia imeshatoa Shilingi Bilioni 2 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Cha kisasa kwani eneo hilo lina watu wengi na wanahitaji huduma ya afya.
Sara pia alifafanua kuhusu sintofahamu iliyojitokeza kuwa eneo la awali lenye ukubwa was hekari 6 Lina mgogoro na kusema kuwa eneo hilo ni Mali halali ya serikari na halina mgogoro wowote.
Aliendelea kusema Kama Kuna mtu anadai eneo ni lake basi aende Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na nyaraka sahihi na taratibu za kisheria zitafatwa.