Mkurugenzi wa Kampuni za Kuzalisha Nguzo za Umeme ya Qwihaya, Leonard Mahenda ameahidi kupeleka nguzo za umeme katika kijiji cha Kilando, Jimbo la Nkasi, Mkoani Rukwa.
Mahenda anayejulikana kwa jina la Qwihaya ametoa ahadi hiyo wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, January Makamba baada ya wananchi kuomba kuletewa nguzo za umeme.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Makamba alimuomba Qwihaya kupeleka nguzo kwa sababu yeye ni mdau wa bidhaa hiyo licha ya kuwa, ni mkandarasi jimboni humo.
“Nimemuahidi Mh Waziri Makamba kuwa tutapeleka nguzo za umeme bure, sisi ni wadau wakubwa na lazima tumuunge mkono mama yetu Rais Samia Suuhu Hassan za kueleka umeme kwenye vijiji,” amesema Qwihaya.
Awali Waziri Makamba aliwahakikishia wananchi wa Jimbo la Nkasi kuwa Serikali itapeleka umeme katika vijiji vyote 27 vilivyobaki.