***************************
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
HARAMBEE ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Mkoa Mwanza yakufanikisha upatikanaji wa fedha za ujenzi wa vituo vya afya vya Baraza hilokatika wilaya saba za Mkoa wa Mwanza, itafanyika Julai 30, mwaka huu.
Harambee hiyo itafanyika katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza naWaziri Mkuu,Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kuhamasishawananchi kuchangia ujenzi huo,hafla inayotarajiwa kuhudhuriwa na waumini naviongozi wa dini, serikali na wadau wa maendeleo.
Akizungumza naWaandishi wa habari leo,Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hasani Kabekealisema Waziri Mkuu,Majaliwa anatarajiwa kuwaongoza viongozi mbalimbali waserikali kuchangisha fedha sh.bilioni 2.7 za ujenzi wa vituo vya afyavinavyojengwa na BAKWATA katika wilaya saba kwa awamu ya kwanza.
Alisema mbali naMajaliwa, pia Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikhe Abubakar Zuber bin Ali Mbwanaatashiriki harambee hiyo akiwaongoza masheikhe kutoka mikoa mbalimbali wakiwemowaumini wa dini za kikristo ili kufanikisha mpango mkakati huo wa miaka mitanokuanzia 2019 hadi 2023.
“Tulimwalika na kumuomba Mh.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Mb) hivyo tunatarajia atakuwa mgeni rasmi wa shughuli yetu adhimu na ya heriya mpango wa miaka mitano ya kusaidia serikali kutoa huduma za afya kwa jamii bila kubagua kwa imani za dini zetu ,rangi wala kabila,”alisemasheikhe Kabeke.
Alisema kuanzisha miradi hiyo walikwenda kujifunza mkoani Shinyanga namna yakutumia rasilimali watu kisha kufanya mikutano ya kuhamasisha michango yaujenzi wa miradi hiyo ya kijamii huku nguvu na imani yao ikijengwa katika umojabaina ya waislamu.
Alhaji Kabeke alisema Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel aliwaungamkono katika jambo hilo wakiwemo waislamu na wasio waislamu ambapo BAKWATAimewafikia watanzania wote ili kuchangia ujenzi wa vituo hivyo saba vya afya nakuvikamilisha.
“Niwaombe wananchi waJiji Mkoa wa Mwanza na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kuchangia ujenzi wa vituosaba vya afya katika harambee itakayofanyika Julai 30, mwaka huu, ilikufanikisha ujenzi huo kwa manufaa ya jamii yetu,”alisema.
Kiongozi huyo wa kiroho alisema baraza hilo halikuwahi kuwa na kituo chaafya hata kimoja jambo lililoifanya jamii ya kiislamu kuwa nyuma katika sualala maendeleo na hivyo ni wakati muafaka wa kuondoa aibu hiyo.
“Hatuwezi kuendelea kuwa watu wa kuchekwa hivyo niwasihi waislamu kilammoja wetu aguswe na kuchangia kwenye mradi huu pia niiombe serikali kuungamkono jitihada hizi zinazofanywa na BAKWATA ni kuondoa majungu na manung’uniko yayojitokezakwa jamii ya kiislamu inapoona serikali ikitoa fedha kwenye taasisi za afyazinazomilikiwa na dini nyingine,”alisema Sheikhe Kabeke.
Mhasibu wa BAKWATAMkoa Said Mrisho alisema mwitikio wa kuchangia ni mkubwa ambapo wanapokea vifaambalimbali vya ujenzi,fedha na mali zingine na kuwaomba wenye ni ya kuendeleakuchangia miradi bado milango iko wizi.
Aidha mshauri wa sheikhe wa mkoa, Alhaji Yusuf Banyanga aliwashukuru wananchi na watanzania walioelewa umuhimu wa afya na kuonyesha nia yakuunga mkono jambo hilo kwa moyo wa upendo.
“Kwa moyo huo niwaombe wananchi wote Julai 30, mwaka huu,waje kutuungamkono katika kutimiza malengo ya kukamilisha miradi ya afya itakayohudumiajamii,tuna matumaini tutafanikisha jambo hilo la heri na tunaweza kuweka rekodi,”alisemaBanyanga
Awali Sheikhe wa Wilaya ya Nyamagana,Othman Ndaki,alisema ana mchango mkubwakatika kuchangia ujenzi wa vituo vya afya na BAKWATA kupitia sheikhe wa mkoaimejikita katika afya ili kutengeneza historia mbili,moja jamii inatengeneza historiaya kumsaidia mtu duniani, pili ni kuwabeba watakapokwenda kuonana naMungu.