Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akitembelea Vibanda kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa wakati wa hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa wakati wa hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa wakati wa hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID, V.Kate Somvongisiri,akizungumzia mradi ulivyowanufaisha vijana wakati wa hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mkurugenzi wa utawala kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Victor Kategere,akitoa maelekezo ya utangulizi wakati wa hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.
……………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinawatambua na kuendelea kutoa mikopo ya Vijana kupitia Mikopo ya asilimia kumi ili kuendeleza juhudi zilizoonyeshwa na wadau wa Maendeleo nchini.
Agizo hilo lilitolewa leo Julai 27,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa kwenye hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022).
Prof.Ndalichako amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya vijana na maeneo mengine yenye lengo la kuleta usawi kwa wananchi.
”Vijana ni nguzo na rasilimali muhimu katika Taifa hivyo Serikali imekuwa ikuchukua hatua za kuhakikisha kwamba inaleta ustawi kwa vijana na kuweka Mazingira wezeshi ya kuweza kupata maendeleo, hivyo kila Halmashauri inawajibu wa kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana kichumi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu.”amesema Prof.Ndalichako
” Tunashukuru Shirika la USAID lakini tunaomba kuangalia namna ya kupanua programu hii ifike kwenye mikoa mingine zaidi ya hii ya awamu ya kwanza,”amesema