MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa
ngazi ya Mkoa wa Tanga 381 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Tanga
Ufundi Jijini Tanga ambako kulikuwa kunafanyika mafunzo hayo kwa siku
21 kulia ni Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Tanga Abogust Mmasa
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa
ngazi ya Mkoa wa Tanga 381 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Tanga
Ufundi Jijini Tanga ambako kulikuwa kunafanyika mafunzo hayo kwa siku
21 kulia ni Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Tanga Abogust Mmasa
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunga mafunzo hayo |
MRATIBU wa Sensa Mkoa wa Tanga Tonny Mwanjota akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo |
Mratibu wa Sensa wilaya ya Lushoto Justin Njuu akielezea namna watakavyotumia mafunzo hayo
Na Oscar Assenga, TANGA.
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim
Mgandilwa amewataka wakufunzi wa zoezi la Sensa ngazi ya wilaya kutumia
mafunzo waliyoyapata kutekeleza jukumu lao kwa ufanisi ikiwemo kujituma
kwa bidii na maarifa wakati wa kuwafundisha wasimamizi na makarani ili
kuweza kupata matokeo bora ya kazi hiyo ya Kitaifa.
DC
Mgandilwa aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa
ngazi ya Mkoa wa Tanga 381 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Tanga
Ufundi Jijini Tanga ambako kulikuwa kunafanyika mafunzo hayo kwa siku
21.
Alisema
katika mafunzo hayo wamejifunza mbinu mbalimbali ikiwemo za kuhoji
wakati wakitekeleza majukumu yao hivyo wamewapatia nyenzo sasa kazi
kubwa walionayo ni kuifanya kazi kikamilifu na ipasavyo.
“Hivyo lazima mjitume kwa bidii na maarifa wakati wa kutekeleza jukumu
lenu la kufundisha wasimamizi na makarani wa Sensa na ndio matumaini
yetu ya kupata matokeo bora ya kazi hiyo ya kitaifa”Alisema DC
Mgandilwa.
“Sensa katika Mkoa wetu ipo mabegani mwenu
mnajukumu la uongozi na dhamana mtakaokuwa mnawafundisha na muwe mfano
kwenye nidhamu,kuzingatia muda na ratibu ya mafunzo na mavazi ,lughu ya
staha na inayoendena na mafunzo yeyu,mheshimu na kuitendea haki dhamana
mliopewa”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Mkuu huyo wa wilaya
alisema katika Sensa ya mwaka huu wanatakiwa kuonyesha umakini na
kuongeza mshikamano haivumilii uzembe wa aina yotote tuwajibike ipasavyo
sipendi kuona watu hawatekelezi majukumu yao kwa kutoa visingizo vya
hapa na pale.
“Nisisitize kwamba ubora wa mafunzo hayo uwe ubora
sambamba na huo mtakaousafirisha kwenye ngazi za wilaya na nimeambiwa
mtakapotoka hapa mnakwenda kutengeneza Jeshi nyengine lenye wasimamizi
9527 ambao ndio watatumika kukusanya taarufa za mkoa na hatime kupata
takwimu bora za idadi ya watu kwenye mkoa wa Tanga”Alisema
Hata hivyo alisema zoezi la Sensa ni muhimu kwa Taifa kikanda na
Kimataifa na litatuwezesha kupata takwimu muhimu zitakazosaidia
kupanga,kupima na kutathimini utekelezaji wa mipango yao ya kimaendeleo
iwe kisketa na mipango ya kitaifa na kimataifa yatakayogusa kwenye
masuala ya kimaendeleo nchini
Awali akizungumza Katibu Tawala
Msaidizi Mkoa wa Tanga Abogust Mmasa alisema baada ya kufungwa kwa
mafunzo hayo sensa itaongoza mkoa huo ile historia iliyofanyika mwezi
wa sita ikifanyika mwezi Agosti mwanzoni itakabidilisha zile takwimu
ionekane Tanga watu wanaelewa wanafanya nini.
Alisema wao ni
watu wa kutimua vumbi maana yake wao haawavuti mkia wao wanaongoza kwa
kila kitu kwa wingi wa Halmashauri na rasilimali zilizopo hiyo hamasa
ikifanye kazi kwenye wilaya,kata na vijiji ili kazi ya Sensa iwe na
ufinisi na mafanikio.