Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati kwenye shule za msingi zenye uhitaji
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya kukabidhi madawati
…………………………………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
MKUU wa wilaya ya Ilemela Hassan Masala amekabidhi jumla ya madawati 1525 Kwa shule za msingi zenye uhitaji.
Akikabidhi madawati hayo, DC Masala ameeleza kuwa kupatikana Kwa vifaa hivyo ni Kutokana na harambee iliyofanyika hivi karibuni wilayani humo lengo ikiwa ni kuboresha miundombinu ya shule za msingi na mazingira mazuri ya Wanafunzi kupata elimu.
Wilaya ya Ilemela ni Moja ya wilaya iliyokua ikikumbwa na wimbi Kubwa la ukosefu wa madawati, Kutokana na hali hiyo Mkuu wa wilaya hiyo Kwa kushirikia na wadau mbalimbali wameweza kupanga mikakati ya kuhakikisha Changamoto hiyo inapungua ama kumalizika mapema iwezekanavyo.
Jamilah Khalifan ni Mkuu wa Division elimu ya msingi na awali ambaye ameeleza kuwa zoezi hilo la uchangiaji wa madawati ni endelevu lengo ni kuhakikisha elimu ya msingi Wilaya ya Ilemala inakua bora na inayostahiki.
Amesema pamoja na kuendelea zoezi hilo bado wilaya ya Ilemela Ina upumgufu wa madarasa1136 hivyo ipo haja ya jamii na wadau mbalimbali kuhakikisha Changamoto hizo zinaondolewa kwani elimu ni msingi kwanza na si vinginevyo.
Amesema ni jukumu la Kila mdau na jamii Kwa ujumla kujitoa Kwa hali na mali Katika kuleta maendeleo.