WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,akiendelea na ukaguzi katika soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 mara baada ya kufanya ziara yake.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,akitoa maelezo kwa wasimamizi wa ujenzi wa Soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 wakati wa ziara yake.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,ya kukagua soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 .
MWAKILISHI wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dickson Kimaro,akipokea maagizo ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,mara baada ya kutembelea soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 .
………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo, ameuagiza Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC kufunga mifumo ya gesi asilia katika soko kubwa la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma ili kuzuia uchafuzi wa mazingira pindi soko hilo likianza kutumika kwa kutumia nishati ambayo sio rafiki na mazingira.
Waziri Jafo ametoa Maagizo hayo leo Julai 26,2022 jijini Dodoma wakati wa ziara katika soko hilo kukagua mifumo ya utunzaji mazingira katika soko hilo ambapo amesema soko hilo linakwenda kuwakutanisha wafanyabiashara zaidi ya elfu sita 6000 hivyo mifumo yote lazima iwe imara ili kuepusha uchafuzi wa mazingira.
Amesema soko hilo ni la kisasa Jijini Dodoma hivyo lazima kuwe na mitambo ya kisasa itakayowasaidia wamachinga kufanya biashara zao
“Hili ni soko la kisasa lazima watu hawa wanaofanya biashara ya upishi kupika vyakula katika soko kujali mazingira ,wanapaswa kujali ajenda ya mazingira kwaajili ya kutumia gesi”,amesema
“Tunatakiwa tuwe na mfumo mmoja hapa wa Natural gesi hili watu watumie kuweka mfumo Mmoja tu wa kulipa bili kuliko kila mmoja kuweka mtungi wake na hii sio nzuri katika suala la biashara”.amesema Jafo
Ameongezea kwa kusema Soko hilo ni la Mfano Tanzania nzima hivyo amemtaka Mkurugenzi Wa Jiji kusimamia suala hilo la Mfumo wa Natural Gas kupatikana katika soko hilo kwa kufanya mawasiliano na Mtendaji Mkuu wa TPDC kufanya utaratibu wa kupata Natural Gas.
“Nakuagiza Mkurugenzi wetu wa Jiji fanya mawasiliano ma Mtendaji Mkuu wa TPDC kuwa tuna soko la kisasa ambalo ni la mfano Tanzania , mueleze tunataka soko hili tupate utaratibu mzima wa kupata Natural Gas”,amesema
“Dodoma ni Makao Makuu ya nchi tuna utajiri mkubwa wa gesi kwa hiyo hilo suala naomba lifikishwe kwa TPDC japo tutaanza na mitungi ya kawaida ya Gesi huku tukiwa tunawasubiri TPDC “.amesema Jafo
Dk.Jafo amesema soko hilo ni lazima liwe na Mtu muhimu wa kusimamia suala zima la mazingira kwa kufanya soko liwe na muonekano mzuri,
sambamba na yote hayo amempongeza Mkandarasi wa soko hilo kwa kufanya kazi vizuri katika kusimamia ujenzi wa soko hilo
Dk.Jafo ametaka kuimarishwa kwa mfumo wa maji safi na maji taka kwani ni maji mengi yatazalishwa katika soko hilo hivyo bila mifumo imara itapelekea mazingira kuchafuka.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema soko hilo linalokwenda kubadilisha maisha ya wafanyabiashara wadogo wadogo kuimarisha mitaji kabla kuwa wafanyabiashara wakubwa.
“Tumeanza utaratibu wa kuwapanga Wamachinga, na zaidi ya machinga 6000 wataingia humu ndani hatuitaji Machinga wengine wabaki huko.
“Na nimesikia kuna maneno yanaendelea kuwa vibanda vingi humu ndani ni vya watu wa Serikalini niwaambie tu kuwa hakuna kibanda cha Mtu wa serikalini humi, vibanda vyote ni vya wamachinga tena wa hali ya chini”.amesema Mtaka
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dickson Kimaro,ameahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo.