Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA ) Habibu Suluo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 26,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara Johansen Kahatano,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 26,2022 jijini Dodoma wakati LATRA wakitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Mkurugenzi wa udhibiti Usafiri wa Reli Mhandisi Hanya Mbawala,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 26,2022 jijini Dodoma wakati LATRA wakitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
Hata hivyo amesema kuwa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika miradi ya kuboresha miundombinu ikiwemo reli na barabara ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kibiashara,kupunguza misongamano mijini na kuvutia uwekezaji.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuhakikisha inaboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo reli na barabara ili kuhakikisha miji inakuwa katika mipangilio mizuri na inavutia.
”Mamlaka imejiwekea mpango mkakati wa miaka mitano, (2020/21- 2024/25), wenye malengo ambayo ni Kuimarisha programu za kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza katika sekta ya usafirishaji ikiwemo VVU/ UKIMWI, Kuimarisha mkakati wa kitaifa dhidi ya Rushwa na mpango wa utekelezaji,Kuimarisha uwezo wa Mamlaka kutekeleza majukumu ya kiudhibiti,Kukuza ushindani na ufanisi katika sekta ya usafirishaji”amesema
Amesema kuwakuboresha uwezo wa kusimamia usalama wa usafiri ardhini,kuboresha mazingira endelevu katika usafiri ardhini na,kukuza huduma bora za usafiri ardhini ili kutekeleza malengo haya ipasavyo, mamlaka imejipanga kuwafikia wananchi kupitia ofisi zake zilizopo mikoa yote Tanzania bara na kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayorahisisha utoaji wa huduma katika sekta zinazodhibitiwa.
Amesema mamlaka imepanga kutoa mafunzo kazini kwa Wafanyakazi Muhimu wa Usalama katika undeshaji wa reli (Safety Critical Workers) kwa TAZARA na TRC ili kuwaongezea ujuzi wa kutimiza majukumu yao kwa weledi.
“Mafunzo ya aina hii husaidia kuwafanya wafanyakazi hao muhimu kuzuia ajali zitokanazo na makosa ya kibinadam (Human Error),Tathmini inaonesha kwamba, makosa ya kibinadamu katika uendeshaji wa shughuli za reli huchangia asilimia zaidi ya 85% ya ajali za treni kwa TRC na TAZARA,”amesema.
Amesema kanuni hizo zitakuwa shirikishi kwa wadau wote wanaohusika,Mamlaka itahakikisha usalama wa treni za mjini (Commuter Trains) unaimarishwa, hasa katika jiji la Dar es Salaam, ambapo TAZARA na TRC zinaendelea kutoa huduma ya usafiri huo.
Aidha amesema Mpango mkakati ni kuwa treni hizi za mjini zinaendeshwa kwa maboresho makubwa ikiwemo ubora wa siti, vitasa vya milango, vishikizi kwa abiria na taa za ndani ya mabehewa.
“Uwepo wa treni za mjini (Commuter) husaidia kupunguza msongamano kwenye mabasi ya daladala,Kwa mujibu wa Kifungu cha 5(g) cha Sheria ya LATRA Na. 3 ya mwaka 2019,
Mamlaka itaendelea kuishauri serikali namna bora ya uendeshaji wa reli kwa njia iliyo salama na kuufanya usafiri wa reli kuwa wa kuaminika,”amesema.
Aidha LATRA imepanga kuendesha semina mbalimbali kwa wananchi na wadau wanaotumia reli ili kuongeza uelewa wa usalama,Hili ni takwa la kisheria kama linavyoainishwa katika Kifungu cha 6(f) cha Sheria ya LATRA Na. 3 ya mwaka 2019.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ilianzishwa kwa Sheria Na. 3 ya Mwaka 2019 ili kudhibiti huduma za usafiri ardhini katika sekta za reli, barabara na waya,Sheria ya LATRA ilifuta Sheria Na. 9 ya mwaka 2001 iliyoanzisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).