Diwani wa Kata ya Budushi wilayani Nzega, Zaituni Kadutu (kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa barabara ya Iyomboitima Budushi, kutoka kwa Mhandisi wa TARURA wilaya ya Nzega, Clinton Gabriel (katikati), kushoto ni mtendaji wa kijiji cha Budushi, Joseph Mayala.
…………………………….
NA VICTOR MAKINDA. NZEGA
Kufunguliwa kwa mtandao wa barabara kwa kuyafikia maeneo ambayo hayakuwa na barabara, unaotekelezwa kwa kasi na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini Nchini, (TARURA) Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora umemkukuna diwani wa kata ya Budushi, Zaituni Kadutu, baada ya kufunguliwa barabara yenye urefu wa kilometa 6.5 inayoiunganisha vijiji viwili vya kata hiyo.
Akizungumzia hali ya miundombinu ya barabara katani Budushi, diwani huyo alisema kuwa tangu Tanganyika ipate uhuru 9 Desemba 1961 kata hiyo haijawahi kuwa na mtandao wa barabara ya kuunganisha makao makuu ya kata na kijiji cha Iyomboitima na kuelekea kuunganishwa na barabara inayokwenda makao makuu ya Wilaya.
“ Nimefurahishwa mno na kasi ya TARURA Wilayani Nzega kwa kutuondolea kero sugu sisi wananchi wa Budushi kwa kutuchongea barabara ambayo ilikuwa ni kilio chetu tangu tupate uhuru.” aliseama Kadutu
Alisema barabara ya Iyomboitima Budushi ambayo imefunguliwa na TARURA itasaidia kupandisha uchumi wa wananchi wa kata hiyo ambao kwa asilimia kubwa uchumi wao unategemea kilimo licha ya kuwa wamekuwa hawana njia ya kupitisha mazao yao kwenda sokoni.
Kadutu aliongeza kusema kuwa kukosekana kwa barabara kwenye kata hiyo kulikuwa kunasababisha wananchi kukosa huduma za msingi kama vile kushindwa kwenda kupata huduma za afya na wanafunzi kushindwa kwenda shule hususani vipindi vya mvua.
Meneja wa TARURA Wilayani Nzega Mhandisi Haruna Mbagalla, alisema wamejipanga kuhakikisha wanafika maeneo ambayo hayajawahi kufikiwa na huduma ya barabara kwani dhima kubwa ya TARURA ni kufungua barabara mpya na kuzihudumia barabara zote hususani za vijijini ili ziweze kupitika msimu wote wa mwaka.
Alisema Wilaya ya Nzega ina maeneo mengi ambayo yanazalisha mazao kwa wingi lakini yalikuwa hayajafikiwa na mtandao wa barabara kazi ambayo imeanza kutekelezwa kwa kipindi hiki cha awamu ya sita.
“Ninamshuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa namna ambavyo ameiongezea bajeti TARURA, inayotuwezesha kuwahudumia wananchi kwa kufungua maeneo ambayo yalikuwa hayajafikiwa kabisa na mtandao wa barabara sambamba na kuzihudumia barabara zote ili ziweze kupitika katika misimu yote ya mwaka. “ Alisema Mbagalla.
Hata hivyo amewashukuru madiwani ambao wamekuwa mstari wa mbele katika miradi inayotekelezwa kwenye kata zao,kwani wmekuwa na mchango mkubwa wa kulekeza wapi panafaa kufunguliwa barabara na uhimu wake tofauti na ilivyokuw hapo awali walipokuwa wakiwasema kwenye vikoa kuwa wmeshindwa kazi.