Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida,
Naing’oya Kipuyo, akizungumza wakati Wajumbe wa Kamati ya Sensa ya Watu na Makazi mkoani hapa walipowatembelea leo Julai 25, 2922 Wakufunzi wa Makarani wa Sensa wanaotarajiwa kuhitimu kesho Julai 26, 2022 katika ukumbi wa VETA mjini hapa ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge anarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WAJUMBE wa Kamati ya Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida wamewatembea
Wakufunzi 216 watakao hitimu mafunzo yao
kesho Julai 26, 2022 ambao watakwenda kutoa mafunzo kwa makarani wa sensa
katika halmashauri zote mkoani Singida.
Wakufunzi hao walianza mafunzo hayo Julai 6, mwaka huu na kesho watayahitimisha
kwa kuhutubiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ambaye
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
Akizungumzia mafunzo hayo Mratibu wa
Sensa Mkoa wa Singida, Naing’oya Kipuyo, alisema yalianza Julai 6 mwaka huu na
kesho ndiyo yatafikia tamati ambapo wahitimu hao nao watakwenda kuyatoa kwa
makarani wa sensa katika wilaya zote.
Kipuyo alisema Mkoa wa Singida unatarajiwa kuwa na makalani na wakufunzi wa
sensa 5,402 ambao usahili wao ulifanyika kuanzia ulai 19, mwaka huu.
Alisema umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na
kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa
utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na
jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;
Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika
utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi
husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.