Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi wakisaini mkataba wa makubaliano wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba akipeana pongezi na Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi wakionesha mikataba mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi wakipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa TGNP mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es SalaamMkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Marco Ndomba akizungumza kwenye hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano na TGNP wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi akizungumza kwenye hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano na DIT wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi (kulia) akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano na DIT wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi wakikagua Maonyesho ya TEHAMA, katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam DIT mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub). Hafla hiyo imefanyika leo Julai 26,2022 kwenye ofisi za DIT Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeingia mkataba wa makubaliano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wa kuanzisha na kuendesha program ya pamoja ya kitovu cha jinsia , uvumbuzi na teknolojia (Establish and Operationalize Gender and ICT innovation hub).
Akizungumza katika hafla hiyo leo Julai 26,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba amesema mktaba huo ambao ni wa muda wa miaka mitatu unalenga kutengeneza vumbuzi na bunifu wa kiteknolojia zenye lengo la kutatua changamoto za kijinsia ili kuharakisha uwezeshaji wa wanawake na usawa wa kijinsia.
Amesema kuna umuhimu wa kukuza sayansi na teknolojia inayozingatia genda ili kuona ni namna gani wanawake pia wanaonesha ubunifu wao ambao ukawa msaada mkubwa kwenye jamii.
“Kupitia mkataba huu DIT itasaidia kuunda mifumo na kuisimamia kimsingi kwa kipindi hiki cha mahusiano pia DIT kupitia wanafunzi na wafanyakazi wataendelea kubuni solution mbalimbali za matatizo ya kinamama”. Amesema
Aidha Prof.Ndomba amesema kuwa katika makubaliano hayo ya miaka mitatu wanategemea kuona mabadiliko makubwa kwa kuwainua mabinti katika sekta ya sayansi na teknolojia kupitia bunifu zao.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi.Lilian Liundi amesema kupitia makubaliano hayo kwa pamoja watashirikiana katika uwekezaji wa wanawake na usawa wa jinsia nchini kwa kutatua changamoto zinazowakabili wanawake kupitia teknolojia kivitendo zaidi.
“Miongoni mwa faida tunazotarajia katika program hii ni pamoja na kuwezesha wanafunzi wa kike kutengeneza bunifu zitakazotatua changamoto za kijinsia, hususan kwa wanawake kuongeza hamasa kwa vijana wa kike kuchukua masomo ya sayansi na teknolojia na kutengeneza bunifu mbalimbali za kimfumo na vifaa zitakazotatua changamoto za kijinsia”. Amesema Bi.Liundi