Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect,hafla iliyofanyika leo Julai 25, 2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara hiyo, Bi. Lugano Rwetaka.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakati wa tukio la utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect leo Julai 25, 2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakionesha nyaraka zilizosainiwa za Makubaliano baina ya Wizara na Kampuni hiyo ya kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect leo Julai 25, 2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, Bw. Tariq Malik (kushoto) wenye lengo la kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect leo Julai 25, 2022 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, Bw. Tariq Malik akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano baina ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tewknolojia ya Habari na Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza leo Julai 25, 2022 jijini Dodoma
Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Jim Yonazi (wa nne kushoto mstari wa mbele) na watendaji kutoka Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Kampunihiyo, Bw. Tariq Malik (wanne kulia mstari wa mbele kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano baina ya Wizara na Kampuni hiyo wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect leo Julai 25, 2022 jijini Dodoma.
…………………
Na Alex Sonna- DODOMA.
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini mkataba wa maridhiano baina ya Wizara na kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, wenye lengo la kuandaa Kongamano la TEHAMA na ubunifu wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo leo Julai 25,2022 jijini Dodoma Katibu Mkuu Kutoka Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi amesema kongamano hilo litasaidia kuchangia uchumi wa kidigitali na litawaleta wadau mbalimbali wenye nia ya kuwekeza katika Tehama.
Dk.Yonazi amesema kuwa Kongamano hilo linalenga kuzidi kukuza matumizi ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kufungua wigo wa mifumo, ubunifu na uwekezaji katika TEHAMA.
“Wadau watakuja kujifunza nchini kwetu na kongamano hilo tunatarajia kufanyia September 7 na 8 mwaka huu linatarajiwa kuwa na wageni takribani 300 watakaokuja kujifunza na hawa watakuja kukutana na wananchi wenye nia ya kuwekeza katika TEHAMA na tunatarajia kuwa na aina nyingi ya watu waliobobea katika sekta hiyo” amesema Dkt Yonazi
Amesema kuwa Tanzania inaunganisha nchi saba za jirani ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na Msumbiji kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo kuwa na fursa kubwa ya kupeleka huduma na kuchichimua uchumi kupitia TEHAMA.
Dkt. Yonazi ameeleza kuwa Kongamano litatoa pia fursa kwa nchi zitakazoshiriki kufanya majadiliano, kujifunza na kuweka mikakati ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuchangia uchumi , kuongeza fursa za uwekezaji, ajira na elimu.
‘Tanzania ina mpango wa kuwa nchi yenye kitovu Cha TEHAMA na ubunifu Katika Eneo la nchi za Afrika Mashariki na kati kwa kuwa Tanzania ni nchi inayounganisha mkongo wa Taifa.’amesema Dk.Yonazi
Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik amesema kuwa Kongamano hilo lilifanyika Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 na kuleta mafanikio makubwa. Aidha, Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano kwa mara nyingine ambapo itapaisha zaidi Tanzania kama kitovu cha mawasiliano.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Bw. Mulembwa Munaku amesema kuwa utiaji saini wa makubaliano hayo ni hatua ya awali ya kuanza maandalizi ya Kongamano kubwa litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi.
Naye Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa, ameipongeza Wizara kwa juhudi za kuweka mifumo imara ambayo itasaidia kutimiza malengo ya Serikali ya kuinua uchumi wa nchi kupitia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
“Uwekezaji huu unatukutanisha na wadau mbalimbali kwani chumi kidigitali ni nyezo muhimu unatukutanisha na wadau mbalimbali na watu ambao wanaweza kuongeza uwekezaji hapa nchini”amesema Msigwa