Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 25,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa,akizungumza wakati Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),ikiwasilisha utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 leo Julai 25,2022 jijini Dodoma.
Mwandishi kutoka Gazeti la Mwananchi Sharon Sauwa,akiuliza swali wakati wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),wakiwasilisha utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 leo Julai 25,2022 jijini Dodoma.
Mwandishi wa habari kutoka Eatv Daniel Mkate,akiuliza maswali wakati wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),wakiwasilisha utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 leo Julai 25,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),akijibu maswali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 25,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
……………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kuhakikisha wakazi wa Jiji la Dodoma wanapata maji safi na salama,Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mradi wa kutoa maji kutoka Bwawa la Mtera unaotarajiwa kutekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 326.
Mradi huo ni miongoni mwa miradi inayopewa kipaumbele katika mwaka wa fedha wa 2022/2023,ambapo kukamilika kwake utaongeza upatikanaji wa maji kwa lita Milioni 130 kwa siku.
Hayo yameelezwa leo Julai 25,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),wakati akieleza utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 mbele ya waandishi wa habari.
“Ujenzi wa Mradi wa kutoa maji Bwawa la Mtera tayari kipo Kukamilishwa kati ya miaka (2 – 2.5) Benki ya Dunia ipo tayari kuufadhili Gharama ya Mradi ni Dola milioni 140 sawa na shilingi bilioni 326b Utaongeza maji lita milioni 130 kwa siku Utaongeza mtandao wa usambazaji maji katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na kuondoa migao ya maji,”amesema
Mhandisi Aron amesema kuwa Mradi huu utahusisha ujenzi wa mabwawa 16 eneo la Nzuguni Utaongeza mtandao wa majitaka usiopungua kilomita 250 na mradi utaunganisha wateja wasiopungua 6,000 pia Utaongeza huduma ya usafi wa Mazingira kutoka asilimia 20 hadi 45.Mradi una gharama ya Tsh.bilioni 161.
“Mradi upo katika hatua za mwisho za kumpata Mkandarasi Mshauri na Mradi wa Majitaka na uboreshaji huduma ya Majisafi kwenye Mji wa Serikali”,
Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DUWASA ipo katika hatua za mwisho kusaini mkataba na Mhandisi Mshauri.
Mradi huu unatarajiwa kugharimu takribani shilingi za Tanzania Bilioni 94 ambazo zimeshatengwa na Serikali Kuu.
Hata hivyo Mhandisi Aron amewataka wananchi kutunza miundombinu ya majisafi na majitaka Lakini pia kutunza vyanzo vya maji kwa kuboresha mazingira hasa upandaji na utunzaji wa miti.
“Pia naomba niwakumbushe wateja wote wa DUWASA kulipa Ankara zao kwa wakati ili kuzuia usumbufu wa kukatiwa maji,” amesema Mhandisi Aron
Akizungumzia kuhusu fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19,Mhandisi Aron amesema Duwasa ilipata Shilnigi Bilioni 1.1 na kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa itawanufaisha takribani wananchi 40,000.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa,ameainisha miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali nchini ikiwemo mradi wa maji katika Mkoa wa Simiyu unaotarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 444.