Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,kwa njia ya simu wakati akizungumza na waendesha bodaboda na bajaji nchini walioshiriki kongamano la kuimarisha ushiriki wa madereva hao katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu jijini Dodoma.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa,akizungumza wakati wa Kongamano la waendesha bodaboda na bajaji nchini walioshiriki kongamano la kuimarisha ushiriki wa madereva hao katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
……………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka waendesha bodaboda na bajaji nchini kuacha kutumika katika Vitendo vya wizi pamoja na kukwapua mizigo ya watu ili kulinda heshima yao.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Julai 24, 2022 wakati alipompigia simu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka kuzungumza na madereva wa bodaboda na bajaji.
Madereva hao walikutana katika kongamano la kuimarisha ushiriki wa waendesha Bodaboda na Bajaji katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu liliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Rais Samia amesema kuwa baadhi ya madereva boda boda wamekuwa wakikwapua mizigo ya watu pamoja na vipochi hasa vya wanawake.
“Tuache tabia ya kukwapuakwapua mizigo ya watu na wizi,msitumie bodaboda vibaya ninyi ni watu muhimu sana na ninawaombea sana hilo muwe walinzi wa amani wa taifa kwani ninyi ni maafisa wa usafirishaji wa taifa msikwapue mizigo ya watu”amesema.
Amewataka waendesha bodaboda na bajaji nchini kutambua kuwa wao ni wasafirishaji wa kitaifa hivyo watumie nafasi hiyo kufanya mambo mema kwa jamii ikiwemo kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi na kuacha ukwapuaji wa mizigo ya watu.
“Mama yenu nipo pamoja na mtakayozungumza, RC ataniletea changamoto zenu ili tuweze kushughulikia,”amesema Rais Samia
Hata hivyo Rais Samia ametoa wito kwa waendesha bodboda na bajaji kushiriki kikamilivu katika suala nzima la sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewaakikishia Madereva bodaboda na bajaji kuwa watatatua changamoto zinazowahusu Dereva bodaboda Pamoja na bajaji zinatatuliwa kwa wakati hili wasione kuwa kazi yao ni kero.
Amesema kuwa wao kama viongozi wa Mkoa wako tayari kusikiliza kero za madereva hao na kuhakikisha zinamfikia Rais Samia kama alivyo ahidi na kutatuliwa kwa wakati.
“Mimi pamoja na viongozi wenzangu tupo hapa kwaajili ya kuhakikisha kila Dereva aliyefika hapa anaeleza changamoto zake, ninyi ni sekta muhimu kwa wananchi wa hali ya chini kutokana na huduma mnayoitoa”,amesema
“Kikao hichi ni cha serikali kwaio lazima tutazichukua tutazipeleka kwenye mamlaka ili wizara husika zifanyie kazi changamoto hizi kero hili ziweze kutatuliwa haraka iwezekanavyo”.Amesema Mtaka
Ameongezea kwa kusema kila Dereva bodaboda na Bajaji asimamie haki ya mwenzake kwa tatizo lolote linalomuhusisha dereva bodaboda au bajaji isipokuwa kuchukua sheria mkononi kwasababu Sheria ni kazi ya Serikali
“Tunajua madereva bodaboda na bajaji mna umoja na hakuna Mwananchi wa kawaida ambae hajui hilo, tunawaomba muwe na umoja kwa kila kitu hii itawasaidia ninyi
“Lakini suala la kuchukua sheria mkononi sio la kwenu hili suala tuwaachie Serikali fateni na kuzingatia sheria mnazowekewa ma Mamlaka husika”.Amesema Mtaka
Awali Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa amewataka madereva bodaboda na bajaji kuwa kipaumbele katika kuamasisha Wananchi kuhesabiwa, na pia kuipongeza kamati ya maandalizi ya Sensa kwa kumteua kijana ambae amekabidhiwa pikipiki kwaajili ya kupita Nchi nzima kuamasisha juu ya Sensa ya Makazi.
“Hili kundi linauamasishaji mkubwa sana na nyie ndio watu ambao tunawategemea katika suala la uamasishaji japo kamati za maandalizi zipo na zimeteua watu katika uamasishaji mkiwemo ninyi dereva bodaboda na Bajaji
“Tunaomba mkawe waamasishaji wazuri tunajua umoja wenu madereva wote Mmoja wenu tumeona amekabidhiwa pikipiki kwaajili ya kutembea Nchi nzima kwaajili tu ya kuamasisha Sensa na Makazi Agosti 2022, na mjue kuwa hii Sensa ni tofauti na uchaguzi”.Amesema Chuwa
Kwa upande wake Mkurugenz Mkuu wa Latra Gilliad Ngewe amesema Bodaboda na bajaji kwa atakayekamatwa na kosa atakayekiri kosa adhabu itakuwa shilingi elfu ishirini na tano na ambaye hajakiri kosa ni shilingi elfu thelathini hadi hamsini.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa njia ya simu katika Kongamano la kuimarisha ushiriki wa waendesha Bodaboda na bajaji katika sensa ya watu na makazi ambapo pia amemuomba Mkuu wa mkoa alitangaze suala hilo katika kongamano hilo.
Amesema faini ya shilingi laki moja itakuwa haipo tena lakini na kuzingatia sheria na kanuni ambazo zinawekwa na wawe wakweli katika kukiri makosa ambayo watakutwa nayo ilikupunguza lawama.