Na Silvia A Mchuruza,Bukoba, Kagera.
SERIKALI imetoa mafunzo kwa wakufunzi zaidi ya 200 watakao enda kuwapatia elimu makalani wa sensa katika maeneo watakayopangiwa.
Mafunzo hayo yametolewa kimkoa katika ukumbi wa Bukoba sekondari ulioko manispaa ya Bukoba mkoani kagera ambapo serikali kupitia kwa mkufunzi wa sensa taifa ndg. Morise Nyatega amesema kuwa kutolewa kwa mafunzo hayo ya siku 21 Ni njia moja wapo ya kurahisisha kazi kwa wale makalani ambao wao kazi yao itakuwa kuwafikia wananchi kwa asilimia mia.
Aidha ndg Morise amesema kuwa kupitia sensa ya majaribio iliyofanyika mkoa wa kagera amejitaidi na wilaya ya kyerwa ndiyo imefanya vizuri zaidi na pia sebsa ya majaribio imewafungua wananchi na kuwapa hamasa ya kushiriki sensa ya mwaka huu itakayofanyika usiku wa kuammia agost 23 nchi nzima.
” Sensa ya mwaka huu Ni ya tofauti na Sensa za kipindi Cha nyuma kwani kupitia hamasa iliyotolewa na serikali kupitia vyombo vya habari wananchi wanaonesha muhitikio juu ya sensa hii”
Ameeleza kuwa mafunzo hayo yanatarajia kukamilika July mwaka huu na kuwataka wanufaika wa mafunzo hayo kuzingatia mbinu walizopewa ili kuweza kufanya kazi nzuri Jambo ambalo litawafanya kutoa taarifa sahihi.
Nae afisa tehama taifa ndg. Elikana Joseph amesema kuwa vifaa vitakavyotumuka yaani vishikwambi avitaitaji mtandao kwa asilimia miamoja Bali vimewekewa mfumo wa Bluetooth ambayo itasaidia kufanya kazi sehemu yoyote ndani ya mkoa wa kagera licha ya kuwepo maeneo ambayo mtandao wake Ni wa kusuasua kwani watatumia mtandao wa TTCL.
Pia ameongeza kuwa Sensa hii ni ya kitofauti kwani inatumia tehema ya kidigitali hivyo serikali imejipanga vyema hata maeneo ambayo mtandao wake unasumbua kwani kalani wa sensa awatatakiwa kutumia mtandao labda wasimamizi ambao watakuwa wanawasilisha kitaifa.
Nao baadhi ya wakufunzi waliopata mafunzo hayo akiwemo bi Jane Novart Rwomile na ndg Jackison Richard wamesema kuwa kupatiwa kwa mafunzo hayo kumewafa kuwa uwelewa wa kipi wanatakiwa kwenda kufanya katika shughuri hii ya kitaifa itakayo fanyika usiku wa kuammia agost 23 mwaka huu nakushukuru serikali kwa kazi inayoendelea kuifanya.