KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga,akizungumza leo Julai 23,2022 jijini Dodoma na washiriki wakati akifunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma yaliyomaliza katika viwanja wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.
Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Gift Kyando,akitoa taarifa ya Mashindano ya UMITASHUMTA 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma yaliyomaliza katika viwanja wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakisikiliza hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga (hayupo pichani),leo Julai 23,2022 jijini Dodoma wakati akifunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma yaliyomaliza katika viwanja wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga,akiwakabidhi Vikombe washindi mbalimbali walioibuka wakati wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma yaliyomaliza katika viwanja wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga,aakiwakabidhi Kombe Walimu wa Jiji la Dodoma walioibuka washindi wa Jumla katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma yaliyomaliza katika viwanja wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.
Walimu kutoka Jiji la Dodoma wakinyanyua Kombe la Ushindi baada ya kuibuka mabingwa wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma yaliyomaliza katika viwanja wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.
WALIMU na Wanafunzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakishangilia mara baada ya kuibuka Mabingwa wa Jumla wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma kwa kujikusanyia alama nyingi kuliko Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma zilizoshiriki mashindano hayo ngazi ya Mkoa mwaka huu.
Wanafunzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakiangalia Makombe yao mara baada ya uibuka Mabingwa wa Jumla wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma kwa kujikusanyia alama nyingi kuliko Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma zilizoshiriki mashindano hayo ngazi ya Mkoa mwaka huu.
…………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
TIMU ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameibuka Mabingwa wa Jumla wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Mkoa wa Dodoma yaliyomaliza katika viwanja wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.
Jiji hilo limeibuka mshindi wa Jumla baada ya kujikusanyia alama nyingi kuliko Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma zilizoshiriki mashindano hayo ngazi ya Mkoa mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kufunga Mashindano hayo leo Julai 23,2022 jijini Dodoma Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga,amewapongeza wanafunzi pamoja na walimu walioshiriki mashindano hayo ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa.
”Nalipongeza jiji la Dodoma kwa kuibuka washindi wa jumla katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa nimeambiwa kuwa Jumla ya washiriki waliokuwa 805 na mmefanya mchunjo na kupata wachezaji 120 wanaounda timu ya mkoa wa Dodoma wanaokwenda kushiriki michuano hiyo kwa ngazi ya Kitaifa, mashindano yatafanyika Mkoani Tabora kuanzia Julai 30,2022”amesema Dk.Mganga
Dk.Mganga amewataka wanafunzi waliochaguliwa kuunda timu ya Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanarudi na ushindi na kuujengea heshima Mkoa wa Dodoma ambao ni Makao Makuu ya nchi.
”Nitashangaa sana mkishindwa na Mkoa wa Katavi au Lindi Kumbukeni mmebeba heshimu ya Mkoa wa Makao Makuu na sisi viongozi wa Mkoa tukipata muda tutakuja kuwaona Tabora ila hata tusikukuja hakikisheni mnarudi na ushindi .”amesema Dkt.Mganga
Aidha amewataka washiriki hao waliochaguliwa kuunda Timu ya Mkoa wa Dodoma kuwa na nidhamu na weledi muda wote watakapokuwa katika mashindano hayo.
”Nataka washiriki wote mnaenda Mkoani Tabora kushiriki Mashindano ya UMITASHUMTA mkawe mfano wa kuigwa katika nidhamu na weledi na kuupa heshima mkoa wetu,hatutaki mkajiingeze kwenye mambo yasiyofaa”
Hata hivyo Dk.Mganga ameseam kuwa ,Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan itaendelea kuimarisha michezo mashuleni ili kusaidia vijana waweze kujiajiri, kuimarisha afya zao.
Awali Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Gift Kyando,amesema kuwa mashindano hayo yaliwakutanisha jumla ya wanamichezo 805 walioweka kambi Shule ya Sekondari ya Dodoma kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma.
”Tumefanya uchambuzi kwa wwashiriki waliofanya vizuri na tumepata Jumla ya washiriki 120 ambao wataenda kuwakilisha Mkoa wa Dodoma katika mashindano ya UMITASHUMITA Mkoani Tabora’amesema Kyando
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2022 ngazi ya Kitaifa yanatarajia kufanyika mkoani Tabora kuanzia Julai 30,2022 .