Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe – Usevya kwaajili ya uzinduzi wa jengo la utawala la Halmashauri hiyo leo tarehe 22 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe iliopo Usevya mkoani Katavi leo tarehe 22 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa Mpimbwe wakati wa hafla ya kuzindua jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe iliopo Usevya mkoani Katavi leo tarehe 22 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitoa zawadi kwa moja ya kikundi cha wanawake waliotoa burudani wakati wa hafla ya kuzindua jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe iliopo Usevya mkoani Katavi leo tarehe 22 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi kituo cha Afya Kibaoni kilichopo Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi leo Julai 22 ,2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Kibaoni kilichopo mkoani Katavi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho leo Julai 22 ,2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi kituo cha afya Kibaoni leo Julai 22 ,2022.
****************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewaasa watumishi wa umma kutumia majengo ya serikali kuhudumia na kutatua kero za wananchi kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 22 Julai 2022 alipozindua Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mpindwe mkoani Katavi, Jengo liligharimu shilingi bilioni 2.9. Amewaasa watendaji na watumishi wote wa halmashauri kuhakikisha fedha zinazopelekwa na serikali katika maeneo yao zinatumika kikamilifu na kwa lengo lililokusudiwa. Amesema umefika wakati wa watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wanapaswa kutoa huduma zilizobora kwa kujitoa na kwa upendo mkubwa.
Aidha Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuharakisha uhakiki na kufanya fidia kwa wananchi wanaostahili ili kuendelea na utekelezaji wa mradi wa barabara ya Kibaoni – Majimoto – Inyonga ambayo imekua changamoto kwa muda mrefu. Pia amesema serikali itashughulikia kikamilifu suala la changamoto ya maji katika halmashauri hiyo na kuagiza wizara ya maji kuhakikisha mradi wa kutoka kata ya Majimoto unakamilika kufikia Novemba mwaka huu.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI mheshimiwa Dkt. Festo Dugange amesema serikali tayari imepeleka bilioni 3.4 kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe na tayari wananchi wameanza kupata huduma katika hospitali hiyo. Aidha ameongeza kwamba serikali ya awamu ya sita imetoa shilingi milioni 300 kwaajili ya ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika halmashauri hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu ambaye pia ni Naibu wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Geoffrey Pinda ameiomba serikali kuanzisha wilaya ya kipolisi katika halmahsuri hiyo pamoja na ujenzi wa gereza ili kuwasaidia wananchi kupata haki zao kwa ukaribu zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mheshimiwa Mwanamvua Mrindoko ameishukuru serikali kwa ujenzi wa majengo saba ya utawala katika mkoa huo ambayo yatawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Awali Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aliweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Kibaoni Halmashauri ya Mpimbwe ambapo amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kusogeza karibu na wananchi huduma zote muhimu zikiwemo huduma za afya. Amewapongeza watendaji wa halmashauri hiyo kwa kutumia fedha za ndani katika kutekeleza mradi huo. Makamu wa Rais amewaasa wahudumu wa afya kuwahudumia wananchi kwa utaalamu na kwa kufuata maadili ya kazi yao.
Makamu wa Rais ameagiza kituo hicho cha afya kukamilika mwezi septemba mwaka huu na tarehe mosi oktoba kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango yupo ziarani mkoani Katavi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero na changamoto za wananchi wa mkoa huo.