Afisa Utumishi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Salum Issa akizungumza kwenye kikao hicho.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza. akiongoza kikao hicho. |
Mpima ardhi Mkoa wa Singida, Sesaria Martin akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ibrahim Magesa akitoa taarifa kwenye kikao hicho.
Afisa Ardhi Wilaya ya Ikungi, Ambross Ngonyani akitoa taarifa.
Afisa Ardhi wa Wilaya ya Itigi, Mfwimi Abraham akitoa taarifa.
Afisa Ardhi Msaidizi Wilaya ya Manyoni, Aron Bisama akitoa taarifaya ufanyaji kazi.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MAAFISA Ardhi katika Halmashauri za
Wilaya Mkoa wa Singida wametakiwa kwenda kutoa ushahidi kwenye baraza
la usuluhishi wa migogoro ya ardhi baada ya kupeleke kesi mbalimbali ili kuzipa
msukumo wa kusikilizwa na kumalizwa.
Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya
Singida, Bahati Colex kwenye kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi mkoa
kilichofanyika mjini hapa leo Julai 22, 2022 katika Ukumbi wa ofisi ya Mkaguzi
na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
“Kumekuwa na changamoto kubwa ya maafisa ardhi kushindwa kuja kwenye
mabaraza ya usuluhishi kutoa ushahidi wa kesi mbalimbali jambo ambalo
linachangia kuwepo kwa kesi nyingi ambazo haziendelei kutokana na kukosekana
kwa ushahidi na kusababisha walalamikaji kukosa haki” alisema.
Afisa Utumishi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Salum Issa
akizungumza na maafisa ardhi hao aliwaomba watumishi wote wa wizara hiyo
kupeleka taarifa sahihi za ajira zao na namba za simu jambo litakalowalahisishia kuwatambua na kuwapata kirahisi pale
wanapotaka kuwapandisha madaraja na mambo mengine.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko
amewapa mwezi mmoja maafisa ardhi hao kuhakikisha wanapima taasisi zote za
serikali ili kukabiliana na changamoto ya uvamizi unaofanywa na baadhi ya watu
kwenye maeneo yanayomilikiwa na serikali.
“Maafisa ardhi mliopo kwenye halmasauri kapimeni taasisi zote za
serikali ili maeneo yote yawe na hati,
hivi sasa taasisi nyingi zikiwamo shule zinavamiwa kwasababu hazijapimwa na
nyie mpo mnaangalia tu,” alisema.
Mwaluko alisema migogoro yote ya ardhi kati ya kijiji na kijiji, wilaya kwa
wilaya na Mkoa kwa Mkoa iorodheshwe ifahamike ili hatua za kuipatia ufumbuzi
ziweze kuanza haraka .
Aliongeza kuwa migogoro ya ardhi kwenye halmashauri tafsiri itolewe ili
iweze kufanyiwa kazi na ile ya mipaka ushauri wa kitaalam utolewe kwani hakuba
sababu ya kukaa na migogoro bila kuitafutia ufumbuzi.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza alisema baadhi ya
maafisa ardhi wamekuwa kikwazo kutokana na tabia ya kuivaa migogoro badala ya
kutoa ushauri.
“Wataalam hatutaki kutoa ushauri wa kuitatua migogoro, tuache tabia ya
kuivaa migogoro, tuhakikushe GN zinapatikana,” alisema.
Alisema suala la migogoro linafahamika kwa watalaam wote wa ardhi hivyo
jukumu lao kubwa ni kutafsiri GN na sio kwenda kueleza wananchi kutafsiri
mipaka.
Katika kikao kazi hicho maafisa ardhi wote wa wilaya walipata fursa ya
kutoa taarifa za utendaji wa kazi zao ambapo zilijadiliwa ili kuona wapi
kulikuwa na upungufu na kuzifanyia kazi
lengo likiwa ni kuboresha zaidi utendaji wa kazi na kuondoa kasoro
zilizokuwepo.