NA
MWANDISHI WETU, MVOMERO
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako amesema kiwanda cha kuchakata nyama cha Nguru Hills kinachomilikiwa na PSSSF
na wabia wengine kimeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya ufugaji.
Mhe.
Profesa Ndalichako ameyasema hayo Julai 21, 2022 alipotembelea Mradi wa
Uendelezaji wa Shamba (Rachi) wa kunenepesha Mifugo na Machinjio ya kisasa wa
Nguru Hills Ranch Wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro.
Alisema
Mradi huo wa uwekezaji uliofanywa na PSSSF na wabia wenza, Kampuni ya Eclipse
Investiment LLC na Kampuni ya Busara Investment LLP ni wa kupongezwa kwani licha
ya kwamba kiwanda kiko kwenye majaribio tayari fursa zimneanza kufunguliwa kwa
wafugaji na vijana.
“Kiwanda
kina uwezo wa kuchinja Ng’ombe 100 na Mbuzi 1,500 kwa siku, soko kwa wafugaji
litaongezeka.” Alisema
Alisema
vijana pia watapata fursa kwa kupata kazi ya kunenepesha Ng’ombe kwa ajili ya
kiwanda. “Kuna vikundi vitatu vya vijana vimepata mkopo kutoka Halmashauri, watafanya
kazi ya unenepeshaji mifugo kwa kuandaa mashamba ya majani kwa ajili ya malisho
ya mifugo.” Alifafanua.
Mhe.
Profesa Ndalichako alionyesha matumaini yake kuwa Mradi utakapoanza kufanya
kazi kwa ukamilifu utaongeza thamani ya mazao yatokanayo na mifugo kama vile
ngozi na nyama yenyewe.
“Ngozi
zitakazopatikana kutoka kwenye kiwanda hiki zitakuwa na ubora wa hali ya juu
kutokana na jinsi nilivyoona mchakato mzima wa uchinjaji.” Alisisitiza.
Alisema
“Ni hatua nzuri na ninaamini Watanzania watanufaika hasahasa wafugaji kwenye
mikoa ya Morogoro na mikoa jirani,”alisema
Alimpongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha uwekezaji wenye tija pia amefungua fursa
nje ya nchi kwani masoko ya kuuza nyama nje tayari yamepatikana ya kutosha na
hivyo bidhaa zitakazozalishwa kutoka kwenye kiwanda hicho licha ya kuuzwa
kwenye soko la ndani pia zitasafirishwa nje ya nchi na kuongeza fedha za
kigeni.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo,
alisema Katika Mradi huo PSSSF inamiliki asilimia 39 ya hisa, huku wawekezaji
wenza Kampuni ya Eclipse Investiment LLC kutoka Oman ikiwekeza hisa asilimia 46
na kampuni ya Busara Investment LLP ya hapa nchini imewekeza hisa asilimia 15.
“PSSSF
imeweka kiasi cha shilingi bilioni 8.3 ambayo ni kama dola milioni 3.9 na
tulikubaliana kwamba Mradi lazima ukidhi mahitaji ya Kimataifa.” Alifafanua.
Alisema
Mradi una miundombinu inayohitajika kama vile eneo la malisho hekta 2,328 lenye
uwezo wa kulisha Ng’ombe 10,000 na Mbuzi 15,000 kwa wakati mmoja.
Kuna
jengo la utawala na jengo kubwa la kiwanda ikiwa ni pamoja na visima vitano vya
maji vyenye uwezo wa kutoa lita elfu 20,000 kwa saa, pia tumejenga barabara za
kuingia hapa ranchi ikiwa ni pamoja na mabwawa.
“Kwa
sasa kiwanda kiko kwenye majaribio ya mwisho (testing and commissioning).”
Alifafanua.
Alisema
soko kuu la bidhaa hizo za nyama ni Mashariki ya Kati.