Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wakulima
wa zao la pamba wameshauriwa kuzingatia kanuni za kilimo ikiwemo kupulizia dawa za kuua wadudu
wanaoshambulia zao hilo ili kuondokana na malalamiko ya kwamba dawa haziui
wadudu na kuachana na tabia ya kusubiri hadi waone wadudu shambani ndipo
wapulizie dawa.
Ushauri huo
umetolewa na Afisa Kilimo Mwandamizi na Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Igunga,
Venance Kankutebe na Afisa Mkaguzi wa
pamba wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Azaria Sanga wakati wa ziara ya Maafisa
Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo wakitembelea wadau wa pamba mkoani Tabora.
Afisa Kilimo
Mwandamizi na Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Igunga, Venance Kankutebe amesema ni
vyema wakulima wakafuata kanuni za kilimo ikiwemo kuzingatia matumizi sahihi ya
viuatilifu na vipulizi kwa wakati mara tum mea unapoota na kuachana na tabia ya
kupulizia dawa baada ya kuona wadudu.
“Tunaendelea
kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu na vipulizi na
katika msimu ujao tumejipanga kikamilifu kutoa viuatilifu na mbegu mapema”,amesema
Kankutebe.
“Tumejipanga
kukabiliana na mdudu Chawajani, Vidung’ata na vidukali kwani hawa ni wadudu hatari
kwenye mmea wa pamba kwa sababu wananyonya maji maji yaliyopo kwenye pamba na
kufanya mmea udhoofike na kusababisha
uzalishaji wa pamba ushuke”,ameeleza Kankutebe.
Naye Afisa
Mkaguzi wa pamba wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Azaria Sanga pia amesisitiza
wakulima kuacha tabia ya hadi waone wadudu ndipo wachukue hatua ya kupulizia
dawa ili kukabiliana na wadudu wanaoshambulia pamba huku akiwasihi kutumia
jembe la palizi linalolokokotwa na ng’ombe
ambalo linaongeza tija kwenye kilimo.
“Tunawashauri
wakulima kuchangamkia majembe ya palizi. Jembe la palizi lina faida nyingi
ikiwemo kupunguza gharama na muda wa kupalilia shamba. Majembe ya palizi yanapatikana Bodi ya pamba na kwa wanaohitaji
majembe haya wawasiliane na maafisa kilimo wa kata husika na wao watawasilisha
majina bodi ya pamba. Lakini pia tunashauri Wakulima wakiona teknolojia za
kisasa katika kilimo wachangamkie ili kuongeza tija”,amesema.
Sanga
ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kuchangamkia kilimo kwani kilimo siyo
adhabu wala siyo utumwa bali kuna utajiri mkubwa wa kumbadilisha mtu kiuchumi
na kubadilisha maisha yake na kuongeza mapato ya nchi akisisitiza kuwa hivi
sasa kilimo kinalipa na ni biashara.
Katibu wa Chama cha Msingi cha Ushirika
(AMCOS) ya Segagi Balimi kijiji cha Ipumbulya kata ya Bukoko wilaya ya Igunga,
Sendama Lutema na Mhasibu wa AMCOS ya Mbogwe wilayani Nzega, Shija Madimi
wamesema miongoni mwa changamoto walizokutana nazo katika msimu huu ni wadudu
waharibifu wa pamba.
Wamesema
wadudu hao akiwemo mdudu hatari chawajani wamekuwa hawafi wanapopuliziwa dawa
hali inayoshusha uzalishaji wa pamba na kuomba serikali kuleta dawa kali zaidi
ili kukabiliana na wadudu hao.
Hata
hivyo wamesema katika msimu huu pamba ni
safi na bei imekuwa ya kuridhisha kwani inauzwa si chini ya bei elekezi ya
serikali ambayo ni shilingi 1560/= na wanaendelea kukusanya pamba kutoka kwa
wakulima.