Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge ,amekabidhi matrekta 10 na Majembe yenye Thamani ya Shilingi Milioni 700 ,kwa Kikundi cha Wakulima wa Mpunga (MBAKIAMTURI) ambapo zana hizo zimewezeshwa na Taasisi ya PASS na KANU Equipment Ltd.
Akizungumza kwenye Halfa hiyo iliyofanyika Stendi ya Mabasi Kibiti ,Kunenge Amewapongeza wanakikundi hao kwa kuja kuwekeza Mkoa wa Pwani.
“Inawezekana kupata Wawekezaji wazuri ndani ya Nchi” amewaeleza kuwa Umoja wao ni nguvu yao na kwani kupitia umoja huo wameeanza kunufaika kwa kupata zana za kilimo”.
Amewaasa kuzingatia Umuhimu wa kilimo cha kitaalam kwa kutumia mitambo ya kisasa na kufuata kanuni za kilimo na kutotegemea kilimo cha Mvua pekee Bali kilimo cha umwagiliaji.
Kunenge,amewataka Viongozi wa Wilaya hiyo kuwasaidia wakazi na Vijana kujiunga kwenye vikundi hivyo na kuboresha maisha.
Ameeleza kuwa suala la Changamoto la Wakulima na Wafugaji linafanyiwa kazi Ipasavyo kwa kusimamia Matumizi bora ya Ardhi. Amewaeleza kuwa Atawasiliana na Waziri wa kilimo ili Ujenzi Miundombinu ya umwagiliaji ijengwe kwenye eneo la mradi huo.
Ameeleza kuwa Katika Mkoa wa Pwani zao la Mpunga linalimwa Rufiji (Nyamweke) ,Chalinze(CHAURU) Bagamoyo (BIDP) , Kibaha Mongomole na Kibiti.
Ameeleza pia mazao mengine ya kibiashara yanayolimwa Mkoani hapo ni pamoja na Katani, Ufuta Korosho, Miwa, Michikikichi, Mpunga, Nazi
Mkuu huyo wa mkoa ,ameongeza kuwa kwa msimu huu Jumla ya Tan 18,266 za ufuta zimeuzwa na kuingizia wakulima Bilioni 57
Naye Mwenyekiti wa Kikundi MBAKIAMTURI Khamisi Mohamed Kambaga hicho akisoma Risala amemshukuru Serikali Mkoani hapo kwa Ushirikiano wa karibu tangu mchakato wa kutafuta eneo la Kilimo hadi leo kukabidhiwa vifaa hivyo. Ameeleza kuwa wapo jumla ya wanakikundi 311 na kwa msimu huu watalima ekari 8000 na wanategemea kupata magunia 120,000.
Ameeleza kuwa wanachangamoto ya Barabara inayoelekea eneo la Mradi, na ameomba kutafutiwa eneo la Ujenzi wa Kiwanda.
Naye Diwani kata ya Mtunda ambapo Eneo la Mradi lipo Mhe Omari Bakari amesema anashukuru kwa mradi huu mkubwa ambao ni wa kipekee katika kata ya Mtunda na amewakaribisha Wawekezaji hao kutoka Mbarari katika ya Kata ya Mtunda na kwamba ni Ardhi nzuri inayozungukwa na mito mingi