Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini ametembelea Ofisi ya Uhamiaji Kituo cha Kirongwe, Wilayani Rorya na kukagua Hali ya Usalama wa Mpaka wa Tanzania na Kenya-Kirongwe tarehe 19/07/2022 ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Mara. Katika ziara hiyo ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe.Juma Chikoka.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amezungumza na Maafisa wa Uhamiaji wa Tanzania na Kenya waliopo katika Mpaka wa Kirongwe,Wilayani Rorya tarehe 19/02/2022 ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ametembelea Ofisi ya Uhamiaji Kituo cha Kogaja ili kujua Hali ya Usalama wa Mpaka wa Tanzania na Kenya-Kogaja tarehe 19/07/2022 ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amelitaka Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na TRA kutoa elimu ya utaratibu wa kutumia vyombo vya moto vilivyosajiliwa na nchi jirani,Kenya ili vitumike kihalali nchini. Aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Kogaja, wilayani Rorya mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ametembelea na kukagua utendaji kazi wa Maafisa Uhamiaji waliopo Mpaka wa Tanzania na Kenya- Sirari na kuzungumza na maafisa wa kituo cha huduma kwa pamoja (OSBP) ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Mara tarehe 20/07/2022.