*******************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Julai 20
MKUU wa mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge ameeleza, ili zoezi la sensa liweze kufanikiwa ifikapo agost 23 mwaka huu, ni lazima kuhakikisha kunakuwepo na utayari wa Wananchi kushiriki zoezi hilo kwa hiari pamoja na usimamizi makini wa kuendesha zoezi zima kwa maana ya vifaa na Wataalamu.
Mkuu huyo wa mkoa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Mkoani hapo alitoa Rai hiyo wakati alipofika kwenye Mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Pwani ambapo jumla ya makarani Wakufunzi 200 kutoka Halmashauri zote wanapatiwa Mafunzo hayo.
“Kama tuna uwezo mzuri lakini Wananchi hawajajitokeza hatuwezi kufanikiwa” Ameeleza Kunenge.
Ameeleza kuwa Mkoa umejipanga kutoa Elimu ya kuhamasisha Wananchi wote waweze kushiriki.
Kunenge alisema ,muhimu kuliko vyote ni Rasilimali watu lazima kuhakikisha kwamba wanapata elimu na kwenda kufundisha wengine.
“Kazi yenu ni muhimu sana ninyi hapa Mtakwamisha au kufanikisha zoezi hili Amewaeleza Kunenge.
Amewaasa kuzingatia kanuni na Taratibu wakati wa Utekelezaji wa zoezi la Sensa. Amewaeleza kuwa ” Dhamana mliyonayo ni kubwa sitarajii kuona watu watakao jitoa kwenye zoezi hilo katikati ya mafunzo na baada ya kupata mafunzo Ameeleza kuwa watakao jitoa hatokubaliana nao”
“Mjifunze muelewe ,mkawafunze wengine sehemu moja katika Mnyororo wa majukumu haya ya Sensa ikiwa haipo sawa tutaharibu zoezi hili kila mmoja atekeleze wajibu wake” amewasisitiza Kunenge.