Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama ya Tanzania Mhe. Angelo Rumisha akitoa mada leo kuhusu Mpango wa Mkakati wa Mahakama wa miaka mitano wakati wa mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi wapya na Wasaidizi wa Kumbukumbu kwenye mafunzo yanayoendelea katika chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bibi Beatrice Patrick akitoa mada leo kuhusu haki na wajibu wakati wa Mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi wapya na Wasaidizi wa Kumbukumbu ambayo yanaendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto
Baadhi ya Mahakimu wakazi na Wasaidizi wa Kumbukumbu wakifuatilia leo mafunzo elekezi yanayoendelea katika chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Ufuatiliaji wa Mahakama ya Tanzania Sebastian Lacha akitoa mada leo kuhusu Utekelezaji wa Mapango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania katika mafunzo elekezi ya Mahakimu wakazi wapya na wasaidizi wa Kumbukumbu ambayo yanaendelea katika Chuo cha Uongozi Lushoto
Na Tiganya Vincent-Mahakama ya Tanzania –Lushoto
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Wibert Chuma amewataka Mahakimu Wakazi wapya kutekeleza majukumu yao utoaji wa huduma ya haki kwenye vituo watakavyopangiwa kwa upendo na haki.
Amesema wapo Mahakimu watapangiwa Vituo vya kazi ambavyo sio vya asili yao au ya wazazi wao na pindi watakapofika sehemu hizo watoe huduma kama vile ambavyo wangetoa kwao.
Mhe. Chuma ametoa kauli hiyo leo Mjini Lushoto wakati wa Mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi wapya na Wasaidizi wa Kumbukumbu ambayo yanaendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama.
“Lazima muelewe kwamba mtakwenda kufanya kazi pengine katika maeneo ambayo sio mlipozaliwa au wazazi wako wanaishi…nendeni mkatoe huduma kwa kuzingatia upendo na haki kama ambavyo mgependa Mahakimu wenzenu watoe haki na upendo katika eneo la kwenu” amesisitiza.
Aidha Msajili Mkuu huyo wa Mahakama amewataka watumishi hao kuwajali wateja wa ndani na nje wanapokuwa wanatoa huduma za haki na pindi wanapowasilikiza wanaohitaji ushauri.
Mhe. Chuma amewasisitiza wawe wanaonyesha huduma zenye upendo kwa wateja wanapoingia katika Ofisi zao kwa kuwajali ili waendelea kuitangaza Mahakama ya Tanzania vizuri ndani nan je.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bibi. Beatrice Patrick amewataka watumishi wapya kuhakikisha kuwa waatifu kwa Serikali iliyopo madarakani.
Amesema hawapaswi kushiriki katika makundi ya mitandao ya kijamii kwa kutoa maoni ambayo yadhalilisha taswira ya Serikali mbele ya jamii.
Aidha Bibi Beatrice amewataka kutumia muda wa wajiri wao uaminifu katika kuwahuduma wananchi ili waweze kupata haki wanazitajaria kutoka Mahakamani.
Amesema kuwa ni makosa kwa watumishi wa umma kutumia rasilimali za serikali ikiwemo magari , muda wa kuwa ofisini kwa maslahi binafsi.