Baadhi ya wandishi wa habari wa Vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba wakiwa katika mafunzo ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika masuala ya siasa yanayofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Chama Cha Wandishi wa Habari Wanawake TAMWA Ofisi ya Pemba(Picha na Masanja Mabula ) Pemba.
…………………………………..
Na Masanja Mabula ,Pemba.
MKURUGENZI Mtendaji wa Chama Cha Wandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar Dr Mzuri Issa amewataka wandishi wa habari kutumia kalamu na taaluma zao kuvunja mifumo ambayo inamkandamiza mwanamke na kumnyima fursa za uongozi .
Alisema bado zipo baadhi ya mila na tamaduni ambazo zinakwaza maendeleo ya mtoto wa kike na mwanamke wa kike na kupitia taaluma na habari wanaweza kuweka uaswa kati ya wanawake na wanaume.
Dr Mzuri aliyadema hao wakati akifungua mafunzo ya wanawake na Uongozi kwa wandishi wa habari za vyombo mbali mbali Unguja na Pemba , yaliyoandaliwa na Mradi wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika masuali ya uongozi na kisiasa.
Alisema kupitia taaluma na vyombo vya habari, wanawake wanapaswa kuandaa vipindi na kuandika habari ambazo zitaleta majibu chanya ya maendeleo na kuongeza hamasa ya wananwake kugombea nafasi za uogozi.
“ Kupitia kalamu zenu hakikisheni mnavunja mifumo ambayo ni kandamizi kwa kundi la wanawake , naamini kalamu zenu ndio silaha pekee ambazo zinaweza kuongeza ushawishi na kuongeza ushiriki wa wanwake katika masuala ya kisiasa”alisema.
Maratibu wa Chama Cha Wandishi wa Habari Kisiwani Pemba Fat-hiya Mussa ni vyema wanashi wa habari kuandika na kutangaza vikwazo ambavyo vinakwamisha mwanamke na kuonyesha njia ya kuzipatia ufumbuzi kwa maslahi mapana ya Taifa.
Alisema pamoja na juhudi ambazo zinachukuliwa na serikali nataasisi binafsi, lakini bado baadhi ya mifumo inakwamisha wanawake kuweza kufikia usawa katika vyombo vya kutoa maamuzi
“Kupitia mafunzo ya leo , hakikisheni mnayatumia kuleta usawa na kufikia yale malengo ya kuwepo na uwiano katika ngazi ya kutoa maamuzi”alifahamisha.
Akitoa manda ya Jinsia na Maendeleo , Mwandishi wa Habari Haji Nassor alisema bado mifumo dume inaendelea kuwakosesha wanawake haki zao za msingi ikiwemo za uongozi.
Mafunzo hayo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika masuala ya siasa na unatekelezwa kwa pamoja kati ya Chama cha wandishi wa habari TAMWA Zanzibar ,Jumuia ya wanasheria wa wanawake Zanzibar – ZAFELA- pamoja na Jumuiya ya kutetezi wa Jinsia na Mazingira Pemba- PEGAO- kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway nchini.