Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama ya Tanzania Mhe. Angelo Rumisha akitoa mada leo kuhusu Mpango wa Mkakati wa Mahakama wa miaka mitano wakati wa mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi wapya na Wasaidizi wa Kumbukumbu kwenye mafunzo yanayoendelea katika chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bibi Beatrice Patrick akitoa mada leo kuhusu haki na wajibu wakati wa Mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi wapya na Wasaidizi wa Kumbukumbu ambayo yanaendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto
Baadhi ya Mahakimu wakazi na Wasaidizi wa Kumbukumbu wakifuatilia leo mafunzo elekezi yanayoendelea katika chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Ufuatiliaji wa Mahakama ya Tanzania Sebastian Lacha akitoa mada leo kuhusu Utekelezaji wa Mapango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania katika mafunzo elekezi ya Mahakimu wakazi wapya na wasaidizi wa Kumbukumbu ambayo yanaendelea katika Chuo cha Uongozi Lushoto
…………………………………….
Na Tiganya Vincent-Mahakama ya Tanzania
Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wanatarajiwa kupewa Komputya mpakato na Vishikwambi (tablets) ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha kuwa na mazingira mazuri ya kuendesha mashauri bila kukwama.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Lushoto na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Mahakama Mhe. Dkt. Angelo Rumisha wakati akitoa mada kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maboresho wa Mahakama wa wa 2020/21 hadi 2024/25 kwenye mafunzo elekezi kwa Mahakimu wakazi wapya na Wasaidizi wa Kumbukumbu yanaendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Amesema kuwa hatua hiyo itawawezesha Mahakimu hao kuendelea na kusililiza mashauri hata mtuhumiwa amekosa gari la kumpeleka Mahakamani kutoka Mahabusu kwa sababu ya kukosekana kwa usafiri siku ya tukio.
Mhe.Dkt.Rumisha amesema hali hiyo itasaidia kuhakikisha mashauri yanaendelea na kuepusha kuharishwa kwa kesi na kusababisha uwepo wa mrundikano wa mashauri katika baadhi ya Mahakama.
Ameongeza kuwa ili kuhakikisha Mahakimu hao hawakwami wakati wanapotumia Vishikwambi hivyo kutatumika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambao wahusika watapapewa wakitoa muda mawasiliano(bando) kwa mwaka mzima ili aweze kufanya vizuri bila vikwazo.
Mhe.Dkt. Rumisho amesema lengo la Mahakama ni kuhakikisha kuwa mashauri yasikilizwa kwa wakati , haki na katika mazingira sawa kwa wote.
Katika hatua nyingine Mahakama kupitia Kitengo cha Maboresho inatarajia kuongeza Mahakama zinazotembea sita ili kusogeza huduma za utoaji haki kwa wananchi wa maeneo ambayo hayana huduma hiyo.
Amesema matumizi ya Mahakama hizo katika Awamu ya Kwanza katika Mkoa wa Dar es sa Salaam na Mwanza yameonyesha mafanikio makubwa kwa kusikiliza mashauri mengi na kutoa maamuzi katika maeneo ambayo hayana huduma hizo kwa njia ya majengo.
Wakati huo huo Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama Mhe. Dkt. Rumisha amesema Mahakama iko katika hatua ya mwisho ya kuwezesha mfumo wa kutafsiri na kuchapisha maamuzi ya mashauri ya Mahakimu na Majaji kuanza kazi nchini Tanzania.
Amesema mfumo huo ambao unatarajia kuanza ndani ya mwaka huu utawawezesha Mahakimu na Majaji wanapomaliza kusoma hukumu , mhusika anapata nakala kwa lugha anayeielewa pale pale