Na John Walter-Manyara
Leo Julai 20,2022 ni kilele Cha maadhimisho ya siku ya Idadi ya watu Duniani.
Maadhimisho hayo yanafanyika Uwanja wa shule ya Msingi Katesh B wilayani Hanang’ mkoani Manyara ambapo mgeni rasmi ni waziri wa fedha Mwigulu Nchemba aliyemwakilisha waziri mkuu Kassim Majaliwa.
Wananchi,viongozi wa dini,Siasa, taasisi na mashirika mbalimbali yamehudhuria.
Makadirio ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya watu ulimwenguni yanaonesha kwamba hadi kufikia mwezi Novemba idadi ya watu inatarajiwa kufikia bilioni 8 duniani,huku India ikitajwa kuipuki China ifikapo 2023.
Hadi sasa nchi zote mbili India na China zina idadi sawa ya watu bilioni 1.4, lakini kulingana na ongezeko la vizazi nchini India huenda likaipiku China kufikia mwaka 2023.
Idadi ya watu inakadiriwa kuwa bilioni 8 kufikia novemba Novemba 15 mwaka huu na inaweza kufika bilioni 8.5 ifikapo mwaka 2030, bilioni 10.4 kwa mwaka 2100, kutokana na kupungua kwa kasi ya idadi ya vifo, ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliotolewa siku ya Jumatatu imesema.
Kauli mbiu inasema” Dunia ya watu Bilioni nane kuhimili wakati ujao ni fursa ya haki kwa wote,shiriki Sensa kwa maendeleo endelevu”.