MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mtera juu ya changamoto ambazo zinawakabili katika suala la Maji wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua mradi huo wa ujenzi wa mradi wa Maji.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Josephat Maganga,akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mradi wa Maji katika Kijiji cha Mtera.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,aakikagua mradi wa ujenzi wa Tanki la Maji katika Kijiji cha Mtera wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua mradi huo wa ujenzi wa mradi wa Maji.
………………………………..
Na Eva Godwin-MPWAPWA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ametoa siku 60 Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kukamilisha ujenzi wa Tanki la maji lenye ujazo lita zaidi ya laki moja katika kijiji cha Mtera Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mtaka ametoa agizo hilo Wilayani Mpwapwa wakati alipotembelea na kukagua mradi huo kutokamilika kwa ujenzi wa Tank hilo na mtandao mzima wa maji Safi na Salama pamoja na kuzungumza na Wananchi wa Mtera juu ya changamoto ambazo zinawakabili Wilayani humo.
Amesema viongozi wa ngazi ya Vijiji na Kata wafanye jitihada kwa kukamilika kwa mradi huo kwa kutekeleza wajibu wao haraka mpaka ifikapo tarehe 25 Septemba 2022 ambapo watakabidhiwa huku wakiendelea kutembelea kwa kujua maendeleo na hali ya mradi
“Tutaongozana na kamati yetu ya usalama na viongozi wa chama na viongozi wa wilaya tutakuja mtukabidhi mradi huo huku tukiwa na Wananchi wa hapa wakishuhudia”,amesema
“Viongozi wa Vijiji na Kata jueni wajibu wenu na kutimiza kwa wakati, sisi tutakuja 25 septemba kupokea mradi wa maji na ninaomba hiyo siku mkurugenzi huandae mkutano unaofanana na mkutano wa Mkoa na wananchi wote tutapanda mlimani”.amesema Mtaka
Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt Fatuma Mganga amesema kumekuwa na sintofahamu kati ya viongozi wa mtera na Wananchi wake na ndio maana kazi haziendi kama ilivyopangwa.
” Hili kazi ziende nilazima kuwe na kamati tatu kamati ya mapokezi,kamati ya ujenzi na kamati ya manunuzi na hapa tutapunguza sintofahamu ya Wananchi na viongozi wake”,amesema
“Kamati hizo tatu zianzishwe na sisi wataalamu tutazisimam na watakao chaguliwa katika hizo kamati twendeni tukafanye kazi kwa kuzingatia misingi na Rasilimali na tunapswa kupata taarifa kwenye kamati” amesema Mganga
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Josephat Maganga amesema amepokea malalamiko ya mradi katika kijiji hicho kuwa mradi unasuasua na baadhi ya miundo mbinu haijakamilika na kugundua usimamizi mbaya wa mradi katika ngazi ya kata.
“Mradi huu ulikuwa unasimamiwa hovyohovyo kwasababu hapakuwa na nyaraka za mradi a niliomba hata moja sikuona rekodi ya watumiaji maji na nilitaka kujua wanaotumia maji lakini sikupata rekodi
” Na niligundua kulikuwa na huitaji wa kurekebisha maeneo mbalimbali ya kurekebisha mradi lakini nikabaini utengenezaji ulikuwa hafifu na mbaya yani kiujumla kamati iliyokuwa hapa ni mbovu”.amesema Maganga