Makama wa Rais wa Jamhuri muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifungua Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Makama wa Rais wa Jamhuri muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.Makama wa Rais wa Jamhuri muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifuatilia Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akizungumza wakati Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Aboud Selemani Jumbe Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvivu Zanzibar akizungumza wakati Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mkutano ukiendelea wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifuatilia Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 19 Julai 2022 amefungua Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini, usimamizi na utunzaji wa mazingira ya Bahari Kongamano lililofanyikia katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 19 hadi 27 Julai 2022.
Akizungumza na Viongozi na washiriki wa Mongamano hilo Makamu wa Rais amesema umoja baina ya Mataifa pamoja na kujitolea ni mambo muhimu yatakayopelekea matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari pamoja na kuepusha kupotea kwa rasilimali hizo.
Amesema ni lazima kuzuia na kupunguza uchafuzi wa Bahari kwa kila namna kuanzia vyanzo vya ardhini hadi baharini.
Ameongeza kwamba unahitajika muongozo endelevu wa biashara ili uchumi wa Bahari uendane na mazingira ya Baharini.
Pia Makamu wa Rais amesema kwa sasa katika kulinda Bahari vinahitajika vitendo zaidi vitakavyokwenda sambamba na sayansi, uvumbuzi na teknolojia pamoja na ushirikishwaji wa wadau wote unaojumuisha vijana na wanawake katika mijadala ambao ni sehemu ya suluhu.
Hali kadhalika Makamu wa Rais amesisitiza kwamba Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kulinda mazingira ikiwemo mazingira ya Bahari kama vile kupiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki inayotumika mara moja, kutenga asilimia 6.5 eneo la Bahari ya Hindi kuwa eneo tengefu la bahari, kudhibiti kwa asilimia 99 uvuvi haramu pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa shughuli za uvuvi wa Bahari kuu.
Amesema umefika wakati wa kutafuta njia sahihi za kudhibiti na kusimamia shughuli zinazofanyika Baharini, pamoja na namna bora ya kuweka uwiano wa kiuchumi, kijamii na kimazingira wakati wa kutumia rasilimali za Bahari.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamiu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Dkt. Sulemani Jafo amesema kuwa Tanzania imepewa fursa na Umoja wa Mataifa ya kuwa mwenyeji na kuratibu Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC.
Asema kuwa kwa sasa dunia inajielekeza katika kuangalia mambo ya Bahari kwa ujumla kama nyenzo muhimu ya kujenga uchumi na masuala mbalimbali ya kijamii.
Amesema Katika mkutano huo kutakua na mambo tofauti tofauti yatakayojadiliwa kwa takribani wiki mbili ili kuona taarifa mbalimbali zinazohusiana na uchumi wa Bahari na utaratibu wa kutoa takwimu mbalimbali za mwenendo wa kiuchumi na kijamii ukihusiana na bahari.
” Mikutano ya Kimataifa inapofanyika kunakuwa na Agenda mbalimbali miongoni mwa jambo chini ya Mkutano huu ni kujadili mambo mbalimbali yanayotokea katika sekta ya uchumi wa Bahari Duniani” amesema Waziri Jafo
Ameongeza kuwa zaidi ya Nchi 22 zimeweza kushiriki mkutano huu ambao washiriki zaidi ya 50 kutoka nchi mbalimbali Duniani wameshiriki ambao utasaidia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu katika masuala ya kibahari , kujengeana uwezo na kujifunza namna Mashirika mbalimbali Duniani yanavyoweza kuratibu masuala ya Bahari na uchumi wake .
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Aboud Jumbe amesema kinachohitajika ni kuendelea kufanya kazi pamoja Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau, watumiaji wa Bahari pamoja na jamii inayoishi pembezoni mwa Bahari kwa ajili ya kuwawezesha kunufaika kiuchumi na mazao yanayotokana na Bahari (Blue economy).
Ameongeza kwamba Wataalam wanapaswa kuzingatia mahitaji ya watumiaji wa Bahari ambao wanaishi pembezoni kwa kuwa wamebeba wajibu wa ulinzi wa rasilimali za baharini.
Awali mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Kitengo cha mambo ya Bahari na Sheria za Kimataifa za Bahari Bi. Alice Hicuburundi amesema kwamba uelewa ni jambo muhimu zaidi katika kulinda na kuhifadhi kwa ajili ya matumizi endelevu ya Bahari.
Amesema matumizi ya sayansi na teknolojia yakiungana na uelewa ndio yanapaswa kuwa msingi wa ulinzi na utawala wa Bahari kwa maendeleo endelevu hasa katika kufikia lengo la 14 la Umoja wa Mataifa.
Madhumuni ya Kongamano hilo ni kuwajengea uwezo washiriki juu ya usimamizi wa Bahari ikiwemo kuonesha hali na mwelekeo wa Bahari, vihatarishi vikuu vinavyoikabili Bahari na mazingira yake, matokeo ya vihatarishi hivyo, na hatua mbalimbali za kupunguza athari hizo.