Na Silvia .A.Mchuruza,Kagera.
Serikali kupitia Wizara ya nishati imesema katika mwaka huu wa fedha 2022/23 Kati ya visiwa 35 vinavyopatikana katika ziwa Victoria kwa mkoa wa kagera visiwa takribani 8 vinatarajia kupokea umeme kutoka katika grid ya taifa.
Akizungumza na wananchi katika mkutanano wa adhara uliofanyika katika Kijiji Cha Bukoki kitongoji nshambya kata Muhtwe wilaya ya muleba waziri wa nishati mh. January Makamba amesema kuwa serikali inajitaidi kuhakikisha inawapatia wananchi waishio visiwani umeme wa huakika kwa kuanzia baada ya mradi wa kufua umeme wa Rusumo kukamilika na miradi mingine ndani ya mkoa
Aidha amewataka wananchi kuendelea kutunza miradi na miundombinu ya umeme inayojengwa kwani ndiyo chanzo kikuu Cha kuwapatia umeme na kuwaondoa wasiwasi wananchi wa visiwani juu ya kutumia gharama kubwa ya kununua unit moja ya umeme kwa wawekezaji ambapo kwa muleba kusini vitapata visiwa 4 na muleba kaskazini visiwa 4.
Pia waziri Makamba ametembelea mradi mwingine uliopo kata ya Bureza wilaya ya Muleba ikiwa Ni kituo Cha kupozea umeme ambapo meneja wa Tanesco wilaya ya Muleba Engineer Lemeck Said amesema kuwa kituo hicho kwa mwaka huu wa fedha 2022/23 kitagharimu shilingi bilioni 8 ikiwa mpaka Sasa mradi umekamilika kwa asilimia 49.8.
“Kwa mwaka wa fedha 2021/22 tulipokea shilingi bilioni 2 na mwaka huu wa fedha tumepokea billion 6 lengo la kujenga laini hii ya umeme Ni kupunguza nguvu kubwa kutoka katika kituo Cha kupozea umeme Kibeta ambapo laini hii itagawa umeme maeneo ya Kamachumu, Muleba mjini pamoja na Ujenzi wa bomba la mafuta Jambo litakalopelekea kupunguza adha ya kukatikatika kwa umeme” Alisema Eng.Said.
Kwa upande mwingine waziri Makamba ametembelea mradi mwingine wa Geita Nyakanazi Substation uliopo wilaya ya Biharamulo maeneo ya Nyakanazi ambapo amesema ameridhishwa na Ujenzi wa mradi huo.
Nae kaimu meneja miradi usafirishaji na usambaji Tanesco Engineer Frank Mashalo amesema mradi wa Nyakanazi baada ya kukamilika utasaidia kuondoa adha ya umeme katika mikoa mitatu ikiwemo Kagera,Geita na Kigoma ambapo mpaka Sasa kituo hicho kimefungwa transformer 2 zenye uwezo wa kugawa katika mikoa hiyo.
” Maeneo ya Kagera yatakayonufaika na mradi wa kituo Cha Nyakanazi Ni pamoja na Biharamulo,Ngara na maeneo mengi jambo ambalo litasaidia Kagera kuondokana na umeme wa Uganda na kuanza kutumia grid ya taifa ambapo amesema mradi huo unajengwa na kampuni ya LARSEN & TOUBRO chini ya mkandarasi ndg. Rajeev Nsomvesh” Alisema eng.Mashalo.